
Mengine mapya na makubwa ya HUAWEI yaliyochukua headlines za dunia March 1 2015

Nilialikwa kuja hapa Barcelona Hispania kuhudhuria maonyesho ya bidhaa za simu duniani ambapo HUAWEI pia wanashiriki, nimekutana na mapya mazuri wakati bado maonyesho haya yanaendelea ndio maana nikasema nikushirikishe na wewe mtu wangu yasikupite haya mazuri kutoka HUAWEI.

Katika kile ambacho dunia nzima inashangaa, Huawei wamezidi kurahisisha maisha kwa kuzindua CarFi 4G LTE. Hivi ni vifaa ambavyo vina kasi hadi 150 Mbps na vitaigeuza gari yako kuwa ‘hotspot’ ya kutawanya internet na kuunganisha vifaa hadi kumi kwa wakati mmoja ambapo hapa Hispania, Huawei wameweka vifaa hivi kwenye magari 400 na vimeonyesha kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu kabisa.
Nakumbuka wakati vinatambulishwa vipya mkurugenzi mtendaji wa Huawei Consumer Business Group Richard Yu amesema “kufuatia mafanikio ya Huawei MediaPad X1 na kurithi muundo wa kipekee wenye kioo kikubwa zaidi, MediaPad X2 inadhihirisha imani na utekelezaji wa ahadi yetu katika kutengeneza vifaa vyenye ubora wa hali ya juu tukitumia teknolojia na uvumbuzi wetu mpya”

Yu akasema tena “Ikiwa ni aina ya pili ya MediaPad, Huawei MediaPad imejikita kwenye matumizi matano yenye umuhimu zaidi kwa watumiaji. Matumizi hayo ni pamoja na ubora wa simu zinazopigwa, application za mitandao ya kijamii, manunuzi mtandaoni, video na picha zenye kuongeza tija kwa mtumiaji, tuna imani kuwa MediaPad itaendelea kuongeza ari kwa watumiaji kupitia muundo wake wa kipekee na uwezo wake wa hali ya juu.”


Katika
vitu ambavyo vimenishawishi kwa asilimia kubwa pia ni hii, unapofanya
mazoezi au kutembea nayo ni nyepesi na wameitengeneza kisasa zaidi
haiwezi kuwa mzigo kwako.




No comments:
Post a Comment