
Kwenye zile story zilizosikika kwenye 255 ya March 5, ni ishu ya muandishi na mtunzi bora wa nyimbo za Bongo Flave msanii
Barnaba kuwaandikia wasanii wenzake nyimbo na kuhofiwa hadhi yake kushuka.
Barnaba amefunguka kuwa hadhi
yake haiwezi kushuka ndio maana kila siku anaendelea kuwa juu kwa sababu
ana moyo wa kutoa kama Dini inavyosema ulichozidishiwa uwape wengine,
anapenda kutoa support na furaha yake ni kuona mtu anasonga mbele kwa
kupitia msaada wake, ameshaandika nyimbo nyingi kama za
Lina,
Recho,
Mwasiti,Vanessa,
Shilole,
Beca,
Baby J na wengine na amekuwa akimudu zaidi kuandika nyimbo zinazoimbwa na wasanii wa kike na kumfanya apendwe sana na wanawake.

Wakati mashabiki wa mziki wa Bongo Flava wakisubiria Tuzo za
Kili Music Award, msanii
AY
amewataka waandaaji wa tuzo hizo kushirikiana na vyombo vya habari ili
kuweza kupata siku nyimbo hizo zilipotoka ili kuepusha migongana kwenye
kupanga vipengele, pia amezungumzia ishu ya video yake ambayo imeanza
kuchezwa Jamaica baada ya bodi ya nchi hiyo kuipitisha.

Story ya mwisho kusikika ni ya star
Ney Wa Mitego ambae wiki hii ameweka wazi majibu yake ya HIV,
Ney
amesema alikuwa hajaumwa muda mrefu lakini hivi karibuni aliumwa na
kwenda Hospitali na kuamua kupima kila kitu kani yeye kama msanii na
balozi wa vijana, anauwezo wa kuwashawishi vijana wenzake kwenda kupima
na kwa sasa ameamua kutulia kwenye mstari mmoja na kuangalia familia
yake.
No comments:
Post a Comment