Lowassa Amjibu Nape Nnauye.....Ahoji ni Kikao gani Cha Chama Kilichomtuma Kutoa Tamko??....Apokea Maandamano ya Vijana 60 Toka Mbeya Wakimtaka Agombee Urais
SIKU moja baada Katibu wa itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Nape Nnauye kutoa kauli ya chama hicho kuhusu makundi yanayojitokeza kumshawishi waziri mkuu mstaafu Mhe Edward Lowassa kugombea urais, kuwa yanaweza kumkosesha sifa kiongozi huyo ya kuwania nafasi hiyo, Mh. Lowassa amejibu kauli hiyo na kudai anashangazwa nayo huku akihoji imetokana na maamuzi ya kikao gani ndani ya CCM.
Lowassa amedai kuwa hana njia ya kuwazuia watu wasimuombe agombee Urais na ametoa ombi kwa wale wote ambao bado wana nia ya kumshawishi agombee nafasi hiyo ya urais, wasubiri kwanza hadi pale chama chake hicho kitakapotoa maelekezo.
Akizungumza
na vijana 60 wa bodaboda kutoka wilaya ya Mbarali, Mbeya waliokwenda
pia kumshawishi agombee nafasi hiyo, mjini Dodoma jana, alisema si vyema
kwa maofisa wa chama kuzungumzia masuala ya wanachama wao kwenye vyombo
vya habari wakati kuna vikao vya chama.
Alisema
watu waliojitokeza na kumshawishi kuchukua fomu za kuwania nafasi hiyo
ya Urais, hajawaita wala kuwalipa chochote kama inavyodaiwa na kwamba
walikuwa wakifuata maneno ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyatoa mkoani
Ruvuma katika sherehe za maadhimisho ya miaka 38 ya Uhuru.
Alisema
katika siku hiyo, Rais Kikwete aliwataka watanzania wawashawishi
viongozi wanaoona wanafaa ili wajitokeze kugombea nafasi hiyo ya Urais.
“Mimi
ni vigumu kuzuia mafuriko kwa mikono. Nazuia mafuriko kwa mikono,
yanakuja mimi nayazuia kwa mikono, nitaweza kweli? Hawa watu sina hoja
nao, sina cha kuwaambia,” alisema Lowasa.
Alisema
tangu makundi hayo yaanze kujitokeza kumshawishi kuchukua fomu mambo
mengi ya ajabu yamesemwa jambo ambalo linamsikitisha na kumshangaza kwa
kuwa endapo kuna mtu wa chama mwenye hoja, ni vyema kuwasilisha kwenye
vikao vya chama badala ya kuzungumza hadharani na kwenye vyombo vya
habari.
Alisema
mambo ya chama humalizwa kwenye vikao vya chama, ambapo majadiliano
hufanyika na mwisho wa siku watu huelewana na kamwe mambo yanayohusu
chama yahawezi kuzungumziwa kwenye vyombo vya habari., televisheni na
redio jambo ambalo ni hatari sana.
“Niseme
mawili tu yanayonisikitisha, wanasema mnakuja nimewaiteni ninawapa
fedha, hela za kuwapa ninazitoa wapi? Mkija hapa nikiwawekea maturubai
ni kosa, mkiwa na viti ni makosa na wanasema nawapikieni chakula, mambo
ya ajabu sana,” alisema.
Alisema
juzi vijana takribani 300 walimtembelea nyumbani kwake, na kushangaa ni
namna ipi angeweza kuwapikia chakula vijana wote hao.
“Ni
vibaya sana kumdhalilisha mwenzako kwamba maisha yake yote akili yake
ni kufikiria tumbo, huyu hana cha kufikiria isipokuwa tumbo, kwa hiyo
mnakuja hapa kwa sababu mnataka Lowasa awape chakula, ni kudhalilisha
watu,” Alisema watu waliomtembelea walikwenda kwa utashi wao wenyewe, kwa gharama zao.
“Sijawaona,
sijawatuma, ama mmeniona huko? Nimekuja kuwashawishi? Nimewahi kuja
huko Mbarali kuwashawishi mje kwangu? Au nimewapeni hela leo mlipokuja
hapa, hata soda zenyewe hamjanywa.”
Aliwataka
wale ambao wanapanga kumshawishi waache kwanza hadi wapate maelekezo ya
chama ili kuepusha migogoro kwenye chama hicho.
“Nina
uhakika tutapata nafasi, jambo moja ninataka kuwapa matumaini ipo siku
watanzania watapata uhuru wa kusema juu ya mtu, iko siku watapiga kura
zao kusema kwa hiyo tungojee hiyo siku.
"Nina uhakika wapo watanzania wengi wanaonipenda kama walivyosema kwa kazi zangu, watapata nafasi ya kusema naam ama hapana, kwa hiyo huyo anayepiga kelele nyingi sijui nitoke chama sijui nifanye kitu gani angoje wanaCCM na watanzania waamue,” alisisitiza.

kitendo cha kufuatwa na makundi mbalimbali ya watanzania kumshawishi
kuwania nafasi ya Urais, kinatokana na ukweli kuwa anaaminika na
kupendwa kutokana na mambo mengi aliyoyafanya.
Kwa
takribani wiki nzima sasa, Lowasa amekua akipokea makundi mbalimbali ya
watu wakiwemo wazee wa CCM, mashehe kutoka Bagamoyo, wanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dodoma (UDOM) na jana waendesha bodaboda kutoka Mbarali
wakimtaka achukue fomu kuwania urais.
Edward
Lowassa akisalimiana na Kamanda wa Vijana Wilaya ya Mbarali ambaye ni
Mfanya Biashara, Ibrahim Ismail Mwakabwangas alipowasili eneo hilo na
ujumbe wake.
Ibrahim Mwakabwangas akizungumza.
Lowassa akipokea salama hizo.
Mwenyekiti wa Bodaboda Mbarali, Yahya Katagara akizungumza.
Kamanda wa Vijana Ibrahim Ismail Mwakabwangas akizungumza na makada wake.
Wednesday, March 25, 2015
CWT yapasuka, Chama kipya cha Walimu chasajiliwa na Wanachama zaidi ya 9,000
CHAMA kipya cha Kutetea Haki na Maslahi ya Walimu Tanzania (CHAKAMWATA)
kimesajiliwa rasmi na kupata cheti cha usajili wa kudumu kutoka Wizara
ya Kazi na Ajira.
Akizungumza na FikraPevu, Katibu Mkuu wa Chakamwata, Mwalimu Meshack Kapange, anasema chama hicho kipya kinaundwa na walimu nchini waliojiondoa kutoka mikononi mwa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT). Kapange amesema mchakato wake wa kukisajili chama hicho ulianza miaka minne iliyopita, hadi hivi juzi kilipopewa usajili wa kuendelea na shuhuli zake kisheria.
“Ni furaha iliyoje kupata usajili huu wa chama chetu cha kutetea haki na maslahi ya walimu? Huu ni ukombozi kwa walimu wanaokatwa asilimia mbili za mishahara yao bila kurejeshewa wanapostaafu,” anasema Katibu Mkuu huyo.
Kuundwa kwa chama kipya hicho kumetajwa na wachambuzi wa mambo kwamba kunaweza kuipasua CWT na pia kutahitimisha ukiritimba wa muda mrefu mrefu wa chama hicho. Aidha, chama hicho kitatoa fursa sasa kwa walimu nchini kuwa na hiyari ya kujiunga na chama ambacho wataona kina maslahi kwao badala ya ilivyo sasa ambapo walimu walikuwa hawana chaguo zaidi ya kujiunga na CWT.
Kwa mujibu wa Mwalimu Kapange, Makao Makuu ya sasa ya chama hicho yatakuwa Jijini Mbeya.
Anasema walimu watakaohitaji kujiunga na chama hicho kipya, watafanya hivyo kwa hiari yao kama sheria za kazi zinavyoelekeza tofauti na CWT ambayo kila mwalimu anayepata ajira serikalini alikuwa analazimishwa kujiunga na kuanza kukatwa fedha zake kutoka kwenye mshahara wake bila ridhaa yake na kinyume cha sheria za ajira.
“Kila mwanachama atachangia asilimia moja tu ya mshahara wake kwa kila mwezi badala ya asilimia mbili kama ilivyo kwa CWT. Wakati mwanachama anapostaafu, atapewa ‘bonus’ kama asante kwa kuchangia Chama,” anasema Mwalimu Kapange.
Mbali na hilo, Kapange anasema Chakamwata kitafanya jitihada za kuwajengea wanachama wake uwezo wa kutambua wajibu wao, haki zao na jinsi ya kuzidai, badala ya kutambua wajibu pekee kama ilivyo ndani ya CWT, kwa maelezo kwamba hakuna wajibu kwa mtumishi yeyote wa umma usiokwenda sambamba na haki yake.
“Tulipokuwa tukiomba usajili kwa mara ya kwanza Mei, 2012, tulikuwa wanachama 400 ingawa masharti ya kisheria ya kuanzisha vyama kama hivi yanataka wanachama 20 tu. Nashukuru kwamba hadi tunapata usajili huu, wanachama wetu wanafikia 9,743, wengi wao wakitokea mikoa ya Mbeya, Iringa, Njombe, Rukwa, Ruvuma, Arusha, Mara, Morogoro, Singida na Kagera,” amesema.
Chama kipya hicho, kabla hakijasajiliwa, kilikuwa kikijulikana kwa jina la Umoja wa Maofisa Elimu Tanzania (UMET). Hata hivyo, uongozi wa muda wa chama hicho ulikaa tena na kukipa chama hicho jina la Chakamwata. Chama hicho kimepewa usajili kwa namba 031, huku cheti chake kikiwa kimesainiwa na Msajili wa Vyama Huru vya Wafanyakazi na Waajiri nchini, Doroth Uiso.
FikraPevu inaendelea kumtafuta Rais wa CWT, Gratian Mukoba, pamoja na maoni ya walimu mbalimbali nchini, ili pamoja na mambo mengine, waweze kuelezea ujio wa chama kipya hicho cha walimu nchini na athari zake katika mstakabali wa mshikamano na utengamano wa walimu nchini katika siku za usoni.

No comments:
Post a Comment