Thursday, March 5, 2015

Hatma ya TV za Kenya kuhusu ishu ya kurusha matangazo ya digitali

runingaaNi takribani wiki tatu tangu kusitishwa kwa matangazo kupitia mfumo wa digitali baada ya Serikali ya Kenya kung’oa mitambo yao ya analojia.
Vituo vitatu vya runinga vilivyozimwa majuma matatu yaliyopita vitarejea hewani leo alhamisi kuanzia saa 12 u nusu saa za Afrika Mashariki .
Vituo hivyo ambavyo vinavyodhaniwa kuwa na ushawishi mkubwa nchini Kenya zimetangaza kuwa zitarejea hewani kuanzia saa kumi na mbili jioni saa za Afrika Mashariki, baada ya majuma matatu gizani.
Vituo hivyo ni Citizen TV, KTN, NTV vimekuwa wakilumbana vikali na serikali kuhusu kuhamia mfumo wa digitali, hadi kwenda mahakamani kutafuta suluhu.
Hata hivyo mahakama iliamua kuwa vituo hivyo havikuwa na la kufanya ila maagizo ya mamlaka inayosimamia masafa na mawasiliano nchini Kenya kwani walikuwa na muda wa kutosha kuweka mikakati inayohitajika kuhamisha matangazo yao kutoka masafa ya analojia hadi yale ya kisasa ya dijitali.
Stesheni hizo ziliomba muda zaidi kuagiza visanduku vya kunga’mua masafa ya digitali kwa wateja wao huku wakilalamika kuwa kampuni zilizopewa leseni kusambaza masafa yao yalikuwa yakitoza ada ya mwezi ilhali hawakuwa wakilipia huduma na matangazo kutoka kwa stesheni hizo.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter  na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter  Facebook

No comments:

Post a Comment