Hii ndiyo akiba ya ngoma za Beyonce zilizoko studio!!
Kama Beyonce
akiamua kufanya albamu moja kila mwaka ambayo itakuwa na nyimbo 10 basi
ana uwezo wa kukaa miaka 10 kuanzia sasa bila kutoa albamu nyingine
yoyote.
Mbali na Beyonce kuna wanamuziki ambao walijiwekea akiba ya nyimbo zao lakini kwa sasa hawapo kama Michael Jackson ambaye kuna nyimbo zake mpaka sasa bado zinafanya vizuri na nyingine zikiwa bado hazijatoka licha ya wenyewe kutokuwepo.
Albamu yake ya mwisho ikiwa ni ya tano inaitwa ‘Beyonce’ na kwa mujibu wa mtayarishaji wake The dream amesema staa huyo ana nyimbo 100 ambazo mpaka sasa hajaamua kuziachia kwa mashabiki wake.

No comments:
Post a Comment