WEMA AUZA GARI LA DIAMOND, ADAI HATAKI KUANZA MWAKA NA GUNDU... NI LILE ALILOZAWADIWA KWENYE BETHIDEI YAKE

‘Diamond Platnumz’ akiwa na aliyekuwa mwandani wake Wema Isaac Sepetu ‘Madam’.
Lile gari jipya aina ya Nissan Murano la staa wa Bongo Fleva, Nasibu
Abdul ‘Diamond Platnumz’ alilompa aliyekuwa mwandani wake, Beautiful
Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ limezua mapya ambapo baada ya kudai
linamchefua sasa anadaiwa kuwa analiuza kwa kigezo kwamba hataki gundu
mwaka huu mpya wa 2015.

KUMBE LIPO KWA DALALI
Habari za kiwango kutoka
kwa mnyetishaji wetu zilidai kwamba gari hilo lipo kwa dalali wa kike
maarufu ajulikanaye kwa jina moja la Tindwa kwa ajili ya kulitafutia
mteja.
NI KISASI?
Ilidaiwa kwamba, Wema
ameamua kufanya hivyo kwa kuwa ana kisasi na hasira kwa Diamond kwa kuwa
jamaa huyo kwa sasa anadaiwa kutoka kimapenzi na staa wa Uganda,
Zarinah Hassani ‘Zari au The Boss Lady’.
“Watu wanadhani Wema anafurahishwa na Diamond kutupia mapicha na Zari baada ya kuwasifia juzikati.
“Ukweli ni kwamba hivi
sasa Wema anakereka sana na jinsi Diamond anavyoweka mapicha yake na
Zari wakiwa sehemu mbalimbali na anaona kuwa na gari ambalo amepewa
zawadi na Diamond ni kujipa kero zisizokuwa na sababu hivyo ameamua
kuliuza,” kilisema chanzo hicho.
HALIJAPATA MTEJA
Mpashaji wetu huyo
alizidi kunyetisha kwamba pamoja na gari hilo kuwa sasa bado liko sokoni
lakini halijapatia mteja wa kulinunua kitu ambacho kinazidi kumkera
Madam.
“Bado gari halijapata
mteja ‘so’ kitendo hicho kinamkera sana Wema kutokana na gari hilo
kutouzika mapema kwa maana kila anapoliona hajisikii vizuri kabisa,”
kilisema chanzo hicho kwa sharti la kutotajwa gazeti kwani ni ‘besti’
mkubwa wa Wema.
WEMA ANASEMAJE?
Baada ya kupewa ubuyu
huo, gazeti hili lilimsaka Wema ambaye alipopatikana alidai yupo bize
akiandaa shoo zake za mkoani Dodoma na Morogoro.
“Ngojeni kwanza nimalize
shoo zangu za mikoani. Kwa sasa nipo Dodoma nikimaliza naenda Morogoro,”
alisema Wema kwa ahadi kuwa atafafanua suala hilo vizuri akitulia.
TUMEFIKAJE HAPA
Diamond alimzawadia Wema
gari hilo lenye thamani ya Sh. milioni 36, siku ya bethidei ya
mwanadada huyo iliyofanyika Septemba 28, mwaka jana.
Siku chache baadaye Wema
alidai kummwaga jamaa huyo huku akieleza kwamba hapendi kuliona wala
kulitumia gari hilo kwani lilikuwa likimzidishia chuki juu ya jamaa
huyo.
No comments:
Post a Comment