Breaking Newzz;Yanga yamtema Rasmi Juma Kaseja
YANGA SC imetangaza rasmi kuachana na mlinda mlango Juma Kaseja, iliyemsajili kwa Sh. Milioni 40 Novemba 8, mwaka juzi.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya
Yanga SC, Jerry Muro amewaambia Waandishi wa Habari leo katika hoteli ya
Zanzibar Ocean View visiwani hapa kwamba, hatua hiyo imefikiwa baada ya
mchezaji huyo kuanza kujiengua katika timu.
“Tumefikia uamuzi wa kuachana na Kaseja, baada ya yeye mwenyewe kuanza kujiengua katika timu,”amesema Muro.
Mwishoni mwa mwaka jana, Kaseja aliwasilisha
barua kwa mwajiri wake, Yanga SC kutoa taarifa ya kuvunja makataba wake,
uliokuwa umebakiza mwaka mmoja.
Katika barua yake, Kaseja alisema sababu ya
kuvunjwa Mkataba huo ni kukiukwa kwa masharti yaliyokubaliwa wakati wa
kusainiwa Novemba 8, mwaka jana.
Barua ya Kaseja iliyotumwa kupitia wakili
wake, Mbamba & Co Advocates, Kaseja imesema wakati wa kusainiwa
Mkataba huo ilikubaliwa malipo ya Sh. Milioni 40 yafanyike kwa awamu
mbili.
Alisema awamu ya kwanza, alilipwa Sh. Milioni
20 baada ya kusaini Mkataba huo, na ikakubaliwa fungu lililobaki
apatiwe Janauri 15, mwaka jana na kwa sababu malipo ya fedha ndio msingi
wa Mkataba wenyewe, kushindwa kulipa fedha hizo kunaondoa uhalali
wake.hivyo, Yanga SC baadaye ilikuja kusema imekwishamlipa fedha zake
zote Kaseja na hana anachodai, ingawa kipa huyo alifungua madai mapya,
akidai anachukiwa na kocha wa makipa, Juma Pondamali hivyo hana amani ya
kufanya kazi.
safi sana
ReplyDelete