Wednesday, January 14, 2015

Mtoto alikuwa analia, baba yake akaamua kumng’ata ili anyamaze!

police_photo
Felipe Deaquino
Matukio ya unyanyasaji kwa watoto wadogo yameendelea kujitokeza kila kukicha, mwanaume mmoja Felipe Deaquino anashikiliwa na Polisi Stamford, Uingereza kwa kosa la kumg’ata usoni mtoto wake mchanga aliyekuwa akilia.
Polisi walifika nyumbani kwa kijana huyo baada ya kupata taarifa za mtoto huyo kunyanyaswa na kumkuta mke wake ambaye aliwaambia Polisi kwamba ana mgogoro na mume wake baada ya kukuta mate usoni kwa mtoto huyo ambaye ana umri wa miezi sita  mchanga mwenye umri wa miezi 6.
Mwanamke huyo na mtoto wake walipelekwa Hospitali baada ya kugundua mtoto huyo alikuwa na majeraha makubwa usoni upande wa kushoto na alikuwa na alama ya kuchomwa moto kwenye kiganja cha mkono ambapo inasemekana kuwa ilisababishwa na sigara.
Deaquino ambaye umri wake ni miaka 18, alikamatwa na Polisi na kuhojiwa akakiri kumng’ata mtoto wake mchanga huku akisema alifanya hivyo kutokana na mtoto huyo kulia, ameshtakiwa kwa makosa mawili ya kushambulia na baadaye akaachiliwa kwa dhamana ya dola 35,000.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter  Facebook

No comments:

Post a Comment