Waandishi wa habari nchini Uganda waandamana kudai mazingira salama ya kufanya kazi.

Waandishi hao waliandamana hadi makao
makuu ya Polisi na kutaka kukutana na mkuu wa Polisi kwa lengo la
kuhakikishiwa mazingira salama ya kufanya kazi, baada ya mwandishi
mwezao kupigwa na kujeruhiwa vibaya na Afisa wa Polisi, Maandamano
yaliyoanza baada ya kikao walichoafikiana kutokuandika habari zozote
kuhusu shughuli za Polisi hadi Afisa aliyefanya tukio hilo akamatwe na
kuachishwa kazi.
“Likuwa
mbaya sana hiyo Journalist hiyo ni watu wa kusave hii nchi yetu sasa
kuona hiyo mambo ya kupiga Journalist tuliona hiyo kitu ni mbaya, sasa
tulisema tunataka tutembee tufike huko Naguru tuone IGP, tumuambie kila
kitu tumeona hapa Journalist tunataka kupigwa sasa watuache tufanye
kazi yetu.“- MWANDISHI
Mwandishi wa habari aliyepigwa na kujeruhuwa akiwa kazini amelazwa katika kumba cha wagonjwa mahututi katika Hospitali ya Msambia, nchini humo.
No comments:
Post a Comment