Mashambulizi ya Paris hayana uhusiano na Uislamu"
Rais Francois Hollande wa Ufaransa amepinga kuweko uhusiano wowote kati
ya wafanya mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni katika mji mkuu wa
nchi hiyo Paris na dini ya Kiislamu.
Akihutubia taifa jana Ijumaa, Rais wa Ufaransa amewataka wananchi wawe
na umoja na kuchukua tahadhari kufuatia kujiri mashambulizi hayo
yakuogofya huko Ufaransa.
Rais Hollande amesema kuwa, wale wote waliohusika na mashambulizi ya
Paris walikuwa ni watu wenye misimamo ya kuchupa mipaka wasio na
mfungamano wowote na Uislamu.
Katika hotuba yake ya jana kwa taifa, Rais wa Ufaransa amewasisitizia raia wa nchi hiyo kuwa macho na kuwa na umoja.
Rais Hollande amewataka wananchi kushiriki kwenye maandamano ya umoja
yaliyopangwa kufanyika kesho kote nchini humo kulaani mashambulizi ya
kigaidi ya Paris. Waislamu wa Ufaransa na katika maeneo mengine duniani
wamelaani mashambulizi ya hivi karibuni katika mji wa Paris.
No comments:
Post a Comment