DIAMOND APEWA ONYO KALI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA
Nasibu Abdul ‘Diamond’.
Mkurungezi
wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka amemuonya msanii
anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’
kutojaribu kujihusisha na utumiaji wa madawa ya kulevya na kusema
akijaribu atapotea.
Mkurungezi wa Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ Asha Baraka.
Akizungumza
na Ijumaa hivi karubini, Asha Baraka ‘Iron Lady’ alisema Diamond
anaweza kufanya vizuri kwa miaka mingi inayokuja lakini akijaribu
kutumia dawa hizo ataishia pabaya.“Tumeona wasanii wengi wa Tanzania ambao awali walikuwa wanafanya vizuri lakini baada ya kujaa sifa na kukutana na marafiki wengi pamoja na makundi wakazama kwenye dawa za kulevya na sasa wanatapatapa na kubaki kulaumu wakati wenyewe wamejiharibia,” alisema Iron Lady.

No comments:
Post a Comment