Saturday, January 31, 2015

STORY kubwa SITA kutoka MAGAZETINI T’Zania tayari nimekusogezea hapa

Leo January 31, STORY kubwa SITA kutoka MAGAZETINI T’Zania tayari nimekusogezea hapa

Glasses & Papaers 
MWANANCHI
Wabunge wameendelea kuwalipua mawaziri, huku wakimtaka Waziri wa Fedha, Saada Mkuya kufukuzwa kutokana na kukiuka Katiba, huku Mbunge Andrew Chenge akikumbana na kadhia ya kudaiwa kuwa anahusika kwenye kila mikataba mibovu, jambo lililosababisha Chenge kusimama na kutoa kauli ya kutaka ‘kuheshimiana’.
Hayo yalitokea Bungeni Dodoma wakati Wabunge wakichangia taarifa za Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) na ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) ya mwaka ulioishia Juni 30 mwaka 2014.
Mkuya alitajwa kubadili matumizi ya fedha zilizotengwa na Serikali kwa ajili ya matumizi mengine, kitendo kinachomaanisha kuwa alivunja Katiba.
Fedha ambazo ziko kwenye ring fence (mfuko maalumu), hazitakiwi kutumika kwa matumizi mengine kwa mujibu wa sheria. Kwa mujibu wa Katiba, Waziri umevunja Katiba kwa mujibu wa ibara ya 135 na ibara ya 136 ni Tanzania peke yake (Waziri Mkuya) unabaki salama. Hupaswi hata kupewa heshima ya kujiuzulu, unafukuzwa kazi,” – Esther Bulaya.
Bulaya, ambaye amekuwa mmoja wa wabunge wachache kutoka chama tawala wanaoihoji Serikali, alisema wizara hiyo imeshindwa kukata fedha kwa ajili ya chai, suti na sambusa na badala yake inakata fedha zilizokuwa ziende kupeleka umeme vijijini.
Bulaya alikuwa akizungumzia Sh180.7 bilioni zilizokusanywa kulipia gharama za mradi kutokana na mauzo ya mafuta ili ziweze kupeleka umeme vijijini.
Wakati wa kuhitimisha mjadala wa ripoti hizo, Naibu Waziri wa Fedha (Sera), Mwigulu Nchemba alikiri kuwa wizara iliyumba katika eneo hilo kutokana na hali ya kifedha ya Serikali.
“Mwaka huu ni hapa tu ambako tuliyumba, (katika) eneo hili la matumizi ya fedha za miradi,” alisema Mwigulu na kuongeza kuwa wizara yake inaandaa utaratibu utakaowezesha makosa hayo kutojirudia.
MWANANCHI
Hofu imetanda kwa wazazi wa watoto ambao wanasoma shule za msingi za Kabasa A na B Wilaya ya Bunda, Mara baada ya kubuka kwa ugonjwa wenye dalili za kupanda ‘mapepo’ ambao unawaathiri wanafunzi wa kike pekee.
Kutokana na ugonjwa huo kuhusishwa na Imani za kishirikina uongozi wa Wilaya uliwataka viongozi wa kijiji kukaa na wazee wa kimila ili kumaliza tatizo hilo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya hiyo, Boniface Maiga alisema Serikali haiamini ushirikina, kwa kuwa tatizo limeanzia kwenye jamii basi jamii hiyo hiyo inapaswa kumaliza tatizo hilo.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Kabasa B alisema ugonjwa huo ulianza kati ya January 21 na 28 huku wakidhani kuwa ugonjwa huo ni Malaria.
NIPASHE
Sakata la uchotwaji wa zaidi ya Shilingi bilioni 300 kwenye akaunti ya Tegeta Escrow limeibuka tena bungeni na kuzua malumbano makali baina ya Mwanasheria Mkuu mpya wa Serikali, George Masaju na Mbunge Tundu Lissu ambaye alimwambia Masaju kuwa ni mshauri wa serikali na si  mshauri wa Bunge kuhusu masuala ya kisheria.
Wakati huohuo Lissu alisema licha ya Bunge kumwondoa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuwafukuza mawaziri, waliochukuliwa hatua ya kufikishwa mahakamani ni watu wadogo waliopewa milioni 80, huku wale waliogawana mabilioni ya fedha wakidunda mitaani.
“Watu wanafanya makosa makubwa dhidi ya umma hakuna hatua inayochukuliwa, waheshimiwa wabunge mnaweza mkauliza, lini mtu  amewahi kuwajibika, nani kachukuliwa hatua, yupi amefungwa, tunajua wanajiuzulu ili wakafaidi matunda ya wizi wao, sheria zetu zinasema wajiuzulu, wafilisiwe, washitakiwe na wakipatikana na hatia wafungwe, nani ameshitakiwa, kufilisiwa au kufungwa?”—Tundu Lissu.
Mbunge huyo alisema kuwa Bunge liliazimia majaji waliohusika na sakata hilo Bunge wawajibishwe, lakini Rais Kikwete hajawachukulia hatua  kwa madai kuwa majaji hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua na mahakama, huku akishangaa nani anayemshauri Rais masuala ya kikatiba na sheria.
“Maazimio ya Bunge lako ni kwamba serikali  ilete taarifa ya utekelezaji maazimio kabla ya kumalizika kwa Bunge la Bajeti lakini hata kabla halijaanza… kanuni zinakataza kumhusisha mheshimiwa Rais kujenga hoja kwa namna ya kejeli, kwa hiyo mimi naomba kushauri kuwa tunapopata fursa ya kuchangia tujikite kwenye hoja yetu na tutumie lugha ya  staha kwa sababu ndivyo kanuni  zinavyoelekeza,” Mwanasheria Masaju.
Lissu aliongeza kuwa ameipata taarifa ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambaye alimwita mrithi wa Jaji Fredrick Werema huku akimweleza kuwa ni mshauri wa serikali na si  Bunge kuhusu masuala ya kisheria ambapo Mwenyekiti wa Bunge, Mussa  Zungu alisimama na kumtaka Lissu kutotumia lugha za vijembe badala yake ajenge hoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Masaju alisimama kuomba mwongozo na kumtaka Lissu kuendelea kuheshimu mihimili mingine kwa kutozungumzia mambo yaliyo mahakamani. 
MTANZANIA
Bibi kizee anayekadiliwa kuwa na umri wa miaka 70 asiyejulikana jina wala makazi yake ameanguka akiwa hajavaa nguo yoyote nyumbani kwa mtu mkoa wa Shinyanga jambo ambalo limehusishwa na Imani za kishirikina.
Suzana Mwandu ambaye ni mwenye nyumba ambayo kikongwe huyo alianguka anasema alimkuta akiwa nje ya jiko llake ambapo baada ya kumsemesha bibi huyo alizinduka na kuanza kuongea vitu visivyoeleweka ambapo mashuhuda walihisi kwamba alikuwa akifanya ushirikina.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa  Waziri Issa amekiri kuwepo kwa tukio hilo ambalo lilikusanya umati wa watu ambapo muda mfupi baadaye Polisi walifika na kumchukua ili kumnusuru bibi huyo kupigwa na wananchi wenye hasira.
MTANZANIA
Mbunge Godbless Lema jana alimshambulia kwa maneno makali Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja kuwa anaweza kuwa anashirikiana na majambazi wanaovamia vituo vya polisi na kupora silaha.
Lema aliliambia Bunge kuwa Chagonja anaweza kuwa anahusika katika matukio ya ujambazi katika vituo vya polisi kwa sababu anataka kudhoofisha utendaji kazi wa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu huku akifananisha taifa na chumba kinachotumiwa na vijana wa kihuni kuishi ambacho hakina utaratibu.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, geto ni mahali ambapo watu wanaishi bila kufuata utaratibu, yaani katika geto, wakati wa kulala anayewahi ndiye anayelala kitandani. Geto chakula kinapopikwa kinaweza kuliwa hata kama hakijaiva, kwa hiyo nchi hii naifananisha na geto kwa sababu watu wanaiba fedha za umma kama wanavyotaka…” Godbless Lema.
“Katika ripoti za Bunge zilizosomwa hapa jana (juzi) zimejaa wizi, kila ukurasa wa taarifa ya Zitto ni wizi tu, wizi tu, hivi huu wizi utakwisha lini? Hata zile bunduki zinazoibwa katika vituo vya polisi zinaweza kuwa ni ‘sabotage’ (hujuma), zinazofanywa na Chagonja dhidi ya IGP,” alisema Lema.
Alisema amefanya uchunguzi wake binafsi uliobaini kuwa Jeshi la Polisi limegawanyika na kwamba haamini kama Rais Kikwete amekwishafanya mabadiliko ya uongozi ndani ya jeshi hilo.
Alisema ikitokea mawaziri wa Tanzania wakapelekwa nchini Tunisia wangeishachukuliwa hatua kali kwa sababu Serikali ya nchi hiyo haiwavumilii wabadhirifu wa fedha za umma.
MTANZANIA
Zitto Kabwe ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi na pia Naibu Waziri wa Fedha jana walialikwa kushiriki mahojiano katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Televisheni ya Taifa (TBC) ambapo katika mjadala huo kila mmoja kumsifia mwenzake kwa utendaji kazi uliotukuka.
Zitto alikwenda mbali zaidi kwa kutangaza kumuunga mkono Mwigulu, ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wanasiasa vijana wanaoendesha harakati za chini kwa chini za kuwania urais baada ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza muhula wake wa pili wa urais mwishoni mwa waka huu.
Katika mjadala huo, ni Mwigulu ambaye ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) aliyeanza kummwagia sifa Zitto kwa jinsi ambavyo amekuwa akitekeleza majukumu yake ya kiuongozi katika nafasi yake ya uenyekiti wa Kamati ya PAC.
Mwigulu alisema Zitto na kamati yake kwa ujumla wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzuri ya kibunge na pia kuishauri vizuri serikali na hasa Wizara ya Fedha.
Zitto alijibu pongezi hizo muda mfupi kabla ya kuhitimishwa kwa mjadala huo kwa kueleza kuwa iwapo Mwigulu ataonyesha nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa baadaye mwaka huu atamuunga mkono, kwa sababu ameonyesha kuwa ni kiongozi mzalendo na mwenye uwezo mkubwa wa kuelewa matatizo ya wananchi na kuyatafutia ufumbuzi.
Alisema ameamua kumuunga mkono kwa sababu yeye anabanwa na umri wake ambao unamwondolea sifa ya kikatiba ya kuwania wadhifa huo, tofauti na Mwigulu ambaye tayari amekwishatimiza miaka 40 inayotajwa kwenye Katiba kama moja ya sifa ya kumwezesha mtu mwenye nia ya kugombea urais kutekeleza matamanio yake hayo.
Alisisitiza kuwa uamuzi wake huo umetokana na tathmini aliyoifanya kuhusu mwenendo wa utendaji kazi wa Mwigulu ndani ya serikali ulioonyesha kuwa ana uwezo mkubwa wa kiuongozi.
Zitto na Mwigulu wameonyesha dhamira ya kuunganisha nguvu zao ili kutekeleza malengo yao ya kisiasa, huku kukiwa na mitazamo mbalimbali ndani na nje ya jamii kuhusu wanasiasa vijana waliokwishaonyesha nia ya kuwania madaraka hayo ya juu ya Dola.
Kitengo cha jarida la The Economist cha The Intelligence Unit ambacho hufanya ufuatiliaji wa siasa za kimataifa, mwishoni mwa mwaka jana kilimtaja Zitto kuwa ni mmoja wa wanasiasa vijana wa kambi ya upinzani ambaye nguvu za kisiasa.
The Intelligence Unit kilieleza kuwa umaarufu wa kisiasa wa Zitto unatokana na nafasi yake ya kiongozi wa kamati nyeti ya Bunge ambayo imekuwa ikiibua mambo mazito na yenye athari katika taifa, hivyo licha ya kuwa na mgogoro na baadhi ya viongozi wenzake ndani ya CHADEMA, bado anao ushawishi mkubwa wa kisiasa kwa wadhifa alionao ndani ya Bunge.

Friday, January 30, 2015

Vanessa Mdee 'Mimi Huwa Sisomi Maoni ya Mashabiki Mtandaoni, Wengi Wanaharibu Hali ya Hewa Kwa Matusi'


Mastaa wengi wamekuwa wakitukanwa na kupewa maneno ya hovyo katika mitandao ya jamii. Mara kadhaa maneno machafu hutolewa baada ya msanii kuandika lolote au kuweka picha.

Mshindi wa Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika Mashariki,Vanessa Mdee ‘Vee Money’ amesema hana utamaduni wa kusoma maoni ya mashabiki wake, kwani alijaribu kufanya hivyo akaona yanampa msongo wa mawazo.

“Sisomi maoni ya mashabiki kwa sababu walio wengi wanaharibu hali ya hewa. Mtu utarudi nyuma kwa kuwaza mambo ya watu, ukiona Nick Minaj ameweka kitu kwenye ukurasa wake haimaanishi kwamba anapenda, ni sehemu ya kazi,” alisema.

“Nilipotaka kutumia rangi katika video yangu nilikuwa nimepanga na isitoshe ilikuwa ni wazo jipya. Sipendi kila kazi yangu ifanane na za wengine, suala la kuwa na vitu vingi linakuongezea, zile rangi mbalimbali ni wazo la watu.

Walio wengi hawakujua video hiyo wala hawafahamu rangi zilimaanisha nini,” alisema Vee Money.

Qoute of the Day
'You've gotta dance like there's nobody watching,
Love like you'll never be hurt,
Sing like there's nobody listening,
And live like it's heaven on earth.'

Mtunis 'Sisi Wanaume wa Dar Hatukuogopa Panya Road, Tulikimbia Tusije Fumaniwa na Wake za Watu Bar'

UTANI KIDOGO: Siunakumbuka Mwita Chacha alivyowaponda wanaume wa Dar, eti hawana lolote wanaenda GYM ili wakamate warembo tu, kwani wameshindwa kuwadhibiti Panya Road  na kukimbia barabarani huku wengine wakijifisha kwenye uvungu wa meza za Bar. Sasa Mtunisy akiwa ni moja kati wa vijana wanoshinda GYM ameibuka na barua hii.

"BARUA hii ije kwako wewe Bw Mwita Chacha sijui toka huko Tarime uliejirekodi na kutuita sisi wanaume wa Dar kuwa ni waoga sana na tunaogopa hata panya rodi tu. Kwa taarifa yako sisi wanaume wa Dar sio waoga kama ulivyotuita na sisi siku ile sio kama tulikuwa tunawakimbia hao panya road bali sisi tulikuwa tunakimbia kuhofia Kufumaniwa na wake za watu tuliokuwa nao kwenye BAR kwani kwenye fujo kama zile lolote huweza kutokea mbaya zaidi zilitokea mapema sana hata no za simu hatujapewa kama huamini kama sisi ni majasiri hamia na mke wako Dar ndani ya miezi mitatu tu uone kama hukumtafuta barabarani na mapanga utadhani wewe ndio panya road na kuishia kuwekwa lupango tu hivi hujiulizi ilikuaje tukawa tunakimbia wakati tuna silaha viunoni kwakua ukifumaniwa hata Bastola huwa kama katoi tu ni hayo Tu Naomba mfikishieni ujumbe huu yule jamaa bye". Mtunisy

VIWANJA VYA BUNGE MJINI DODOMA LEO


 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akifurahia jambo  na Mbunge wa Viti Maalumu, Zainabu Vullu katika viwanja vya bunge  walipohudhuria kikao cha pili cha mkutano wa 18 wa Bunge mjini Dodoma jana.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa akielezwa jambo na  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi katika  viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana.
 

Thursday, January 29, 2015

Thursday, January 29, 2015

BUSARA ZA MICHAEL WAKUDATA.

BINTI WA MIAKA 22 ASHINDA MILIONI 100 ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM

Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akifafanua jambo kuhusiana na mshindi wa shilingi Milioni 100/-kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na kampuni hiyo ambapo Mkazi wa kilolo mkoani Iringa Bi.Uwezo Magedenge aliibuka na ushindi wa kitita hicho katika droo ya 14 iliyochezeshwa jijini Dar es Salaam leo,Wengine ni Msimamizi wa Michezo ya Kubahatisha Tanzania Mrisho Millao(Kushoto) na Afisa wa kampuni hiyo Pristin Lyatonga.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544.

Mkazi wa Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Uwezo Magendenye (22) , leo ameibuka mshindi wa kwanza wa shilingi milioni 100 katika droo ya kumi na nne ya promosheni ya Jaymilioni inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

Magedenge binti mwenye umri wa miaka 22 ambaye ni mhudumu wa mapokezi katika nyumba ya wageni ya Luganga Lodge iliyopo wilayani Kilolo amesema kuwa amepokea taarifa hizi kwa furaha akiwa kazini na amefurahia ushindi huu ambao anaamini utabadilisha maisha yake kwa kiasi kikubwa.

“Katika maisha yangu nimeishapitia mambo mengi nahangaika na maisha hadi kufikia hapa nilipo nikiwa mhudumu kwenye nyumba ya wageni.Kwa ushindi huu naamini nitafungua shughuli zangu za biashara ikiwemo kuanzisha biashara ya maduka ya M-Pesa pia kufungua nyumba yangu ya kulala wageni na kusaidia ndugu zangu ambao wanakabiliwa na changamoto mbalimbali za maisha”.Alisema.

“.Nashukuru Vodacom kwa kuleta promosheni hii ambayo naamini itabadilisha maisha yangu na namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuniona na kusikiliza sala zangu .

Aliongeza kuwa kwa muda mrefu amekuwa akishiriki kwenye promosheni mbalimbali na hajawahi kufanikiwa kwa ushindi huu anaamini kuwa promosheni hizi hususani za Vodacom ni za kweli na amewataka wateja wote kushiriki ili kutopoteza bahati zao za kujishindia mamilioni ya fedha na kubadilisha maisha yao.

Akiongea muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi, Mkurugenzi mtendaji wa Vodacom Tanzania,Rene Meza amempongeza mshindi na kuwahimiza wateja wote kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za kushinda pia alisema kuwa njia nyingine ya kushinda ni kutuma neno AUTO kwenda namba 15544 iwapo simu haina fedha ambapo mteja akiweka fedha anakatwa shilingi 300/-.

Naye Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania alisema kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja 2 wamekwishajishindia milioni 10 na wateja watano wameishajishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.

“Promosheni hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya kumi na nne hivyo bado kuna mabilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa kufanya ni kuhakikisha kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka na ushindi kwenye droo ya siku kwa kutuma neno Jay kwenda namba 15544.

ZIARA YA MBUNGE JOSEPH MBILINYI ( SUGU) ILIYOFANYIKA WILAYANI ILEJE


 Mh: joseph mbilinyi akicheza ngoma ya  asili na wananchi


 Picha ikimuonyesha mh: joseph mbilinyi akiwa jukwani akiwahutubia mamia ya watu wilayani ileje

CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA YA RUNGWE KIMEINGIA KATIKA KASFA NZITO BAADA YA KUDAIWA KUUTEKA MSAFARA WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA KUWAJERUHI KWA MAPANGA,MARUNGU NA NONDO.





 Ndg. Max Mwasomola ni Mmoja wa waliojeruhiwa aliyeng'olewa jino na kukatwa kucha
 
 Mwenyekiti wa BAVICHA taifa Ndg. Patrick Ole Sosopi akimtakia hali Max Mwasomola aliyeng'olewa jino na kukatwa kucha na viongozi wa CCM.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Rungwe Mbeya kimeingia katika kashfa nzito baada ya kudaiwa kuuteka msafara wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)  kuwatesa na kuwajeruhi kwa mapanga,rungu na nondo huku wakiwang’oa meno na kucha viongozi watatu wa chadema.
Akizungumza na Tanzania daima leo (jana) kamanda wa ulinzi na usalama wa jimbo la Rungwe Magharibi Reonad Joseph alisema tukio hilo lilitokea saa moja usiku wa kuamkia leo wakiwa njiani wakitokea kata ya Lufilyo walikokuwa wakifanya mkutano.
Alisema Chadema ilikuwa kwenye ziara wilayani humo ambayo iliongozwa na naibu mwenyekiti wa baraza la vijana (BAVICHA) huku Chama cha Mapinduzi wakifanya ziara iliyokuwa chini ya mwenyekiti wao wa mkoa wa Mbeya…… na kwamba wananchi walikuwa mwakisusia mikutano yao na kujaa katika mikutano ya Chadema.
Kutokana na hali hiyo Chama Cha Mapinduzi kupitia makada wake walipanda kuuteka msafara wa viongozi wa Chadema wakati wa kurejea Tukuyu mjini maeneo ya kata ya Mbambo walilazimika kubadirisha njia ili kuwanusuru viongozi wa kitaifa na hatimaye wakafanikiwa kuwateka viongozi watatu waliokuwa na pikipiki.
Aliongeza kuwa baada ya kuwateka viongozi hao walianza kuwapiga na kufanikiwa kuwakata na mapanga maeneo mbalimbali ya sehemu za mwili wao na kuwang’oa meno na kucha  ambapo walikuja okolewa na wananchi wa eneo hilo na hatimaye kuwakimbiza katika hospitali ya wilaya kwa matibabu na kutoa taarifa kwa jeshi la polisi wilayani humo.
Katibu wa siasa itikadi na uenezi wa jimbo hilo,Grece Kalambo alishangazwa na hatua ya Chama hicho kuendesha operesheni hiyo,na kuwa siasa sio ugomvi wanatakiwa kushindana kwa hoja na si kuleta vita pamoja na kuwa wananchi tayari wamekichoka chama hicho wanatakiwa kujitathmini upya.
Mwenyekiti wa jimbo hilo,Juma Kibo alisema chanzo cha Chama hicho kuendesha utekaji kwa viongozi wa chadema ni kutokana na wananchi kususia mikutano yao na kujaa kwenye mikutano ya Chadema kutokana na kuwa na maelezo na sera nzuri zinazowavutia wananchi kila kona.
Kibo aliwataja baadhi ya viongozi waliotekwa na kuteswa kwa kukatwa na mapanga,kung’olewa meno na kucha ni mwenyekiti wa bavicha wilaya,Gastor Mwakasege,aliyepigwa lungu begani na kupokonywa pesa Tsh,laki 2.9 pamoja na simu,Jonathani Mwakyusa aliyekatwa mguu na kupokonywa viatu vyenye thamani ta Tsh,30,000,na Max Mwasomora aliyeng’lewa jino na kucha.
Makamo mwenyekiti wa Baraza la vijana (BAVICHA)Taifa Patrick Olle Sosopi mbali na kushangazwa na tukio hilo alisema utekaji huo ulimlenga yeye na kuwa anaipongeza kamati ya ulinzi na usalama wa jimbo hilo kwa kutambuo hilo na kunibadirishia njia.
Kutokana na hali hiyo Sosopi alilishutumu jeshi la polisi wilayani humo kwa kutowapa ulinzi baada ya kuwapa taarifa juu ya uwepo wa utekaji huo na kwamba majeruhi walipelekwa hospitalini na kwamba wamefungua jarada la kesi nambaTUK/IR/115/2015 shambulio na faili la kesi ni CC NO-9/2015.
Sosopi alisem wameliachia Jeshi la polisi lifanye kazi yake na kuwa kama kutakuwa na upendeleo kwa Chama cha mapinduzi basi watatoa maamuzi magumu juu ya wahusika wote kwa kuwa CCM inakila kitu lakini Chadema wanategemea nguvu ya umma,’’kwa sasa tunaendelea na ziara katika maeneo yote tuliyoyapanga’’alisema.
Mwenyekiti wa umoja wa vijana (UVCCM) wilayani humo,Arbat Kawonga mbali na kukili kuwepo na tukio hilo alisema Chama chake hakihusiki na tukio hilo.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilayani humo,Ally Mwakalendile alisema yeye hakuwepo wakati tukio hilo likitokea na kuwa hawezi kuzungumza chochote.
Jeshi la polisi wilayani humo limekiri kuepo na tukio hilo na kuwa tayari linamshikilia dereva wa gari aina ya Noah lenye namba T,408 DBM lililotumika kwa shughuri hiyo na kwamba dereva wa gari hilo amepelekwa mahakamani leo na kufunguliwa shitaka hilo.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya hiyo Dkt,Sungwa Ndagambwe amekiri kupokea majeruhi hao na kuwa wanaendelea kupatiwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Mwisho.

Saturday, January 24, 2015

UKAWA yatangaza kususia Kura ya Maoni


Vyama vya Siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi nchini Tanzania (UKAWA) jana vimetangaza rasmi kuwa vitasusia kushiriki kura ya maoni, zoezi ambalo ni hatua muhimu katika mchakato wa kupata Katiba mpya na ambalo litafanyika April 30 mwaka huu.
 
Viongozi wakuu wa vyama vinavyounda UKAWA wametangaza uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam , ambapo Mwenyekiti Mwenza wa UKAWA Profesa Ibrahim Lipumba ameelezea sababu za wao kutoshiriki na namna watakavyoshawishi wananchi nao wasishiriki zoezi hilo.
 
Ameelezea sababu kubwa ya kususia zoezi hilo kuwa ni kwamba mchakato wa kuipata Katiba Inayopendekezwa haukuwa halali, na hivyo Katiba Inayopendekezwa si halali na hivyo hawawezi kushiriki katika kitu haramu..
 
Lipumba amesema kuwa maandalizi ya kuandikisha wapiga kura hayaridhishi, na kwamba vifaa vya BVR vilivyopo nchini hadi sasa ni 250, makubaliano ya tume ilikuwa ni kuwa na vifaa 15,000, lakini serikali ilikubali kugharamia vifaa 8000, na kwa mujibuwa NEC vituo vya kupigia kura vinatarajia kuwa 40,015 kwahiyo ni ndoto kuwaandikisha wapiga kura milioni 23 hadi kufikia April 30.
 
Sababu nyingine iliyotajwa ni kwamba wananchi bado hawajaielewa Katiba Inayopendekezwa, na serikali haifanyi juhudi zozote kuchapisha nakala za katiba hiyo ili wananchi waielewe.
 
Emanuel Makaidi amesema “Haramu haiwezi kuzaa halali, ingawa halali inaweza kuzaa haramu,…” kwahiyo wao walisusia mchakato ambao ulikuwa haramu, hawawezi kuunga mkono zao la mchakato haramu."
 
Freeman Mbowe: “Tumejitoa na hatutarudi kwa gharama yoyote, BVR watu hawajui na hakuna maandalizi yoyote…… CCM wanataka kuliingiza taifa kwenye machafuko."
 
Wenyeviti hao wamesema kuwa kama serikali italazimisha mchakato huo, basi itegemee vituo vya kupigia kura siku hiyo kutokuwa na watu kabisa, hali ambayo huenda ikasababisha machafuko.
 
Wakati UKAWA wakitangaza kususia Kura ya Maoni, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nacho kimeitaka serikali kusitisha zoezi hilo kwa madai ya mapungufu kadhaa ikiwemo maandalizi hafifu, pamoja na mapungufu katika sheria ya kura ya maoni.
 
Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho Bi. Hellen Kijo-Bisimba amesema kuwa udhaifu huo wote unalenga kulinufaisha kundi fulani la watu katika jamii.

Thursday, January 22, 2015

NAPE: CCM HAITARUHUSU WANUNUA URAIS KUPENYA 2015



> . Asema wanapoteza muda na pesa zao
>. Awataka wakumbuke salaam za mwaka mpya 2015 za CCM.
>. Ajivunia uzoefu wa CCM kudhibiti wasio waadilifu
>. Atamba CCM kufanya vizuri uchaguzi mkuu 2015.
>. Awataka Watanzania kuiombea nchi ipate kiongozi mwadilifu.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Ndg. Nape Nnauye amewaibukia tena wasaka urais ndani ya CCM na kudai kuwa Chama hicho hakitatoa mwanya kwa wanaosaka uteuzi huo kwa kununua wajumbe mbalimbali wa vikao husika.

Nape ameyasema hayo jana kwenye  mafunzo kwa wachungaji wote wa huduma ya Efatha nchini yaliyofanyika Kibaha mkoani Pwani. Nape alikuwa akitoa mada inayohusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii.


Pamoja na Nape


ambaye aliwakilisha CCM kwenye mafunzo hayo walikuwepo watoa mada wengine kutoka vyama vingine vya upinzani nchini.

Akizungumzia mada ya nafasi na uhusiano wa CCM ndani ya jamii, Nape alisema historia ya Chama hicho ambayo haiwezi kwa vyovyote kufanana na ya chama chochote kilichopo au kijacho nchini ni moja ya sababu kubwa ya Watanzania kuendelea kukiamini Chama hicho. Aliongeza kuwa sababu kubwa ya pili ni misingi ambayo Chama hicho kinaiamini ambayo ndio imelifanya taifa la Tanzania kuwa taifa.


Nape alisema CCM ipo kila kona ya nchi na hivyo inamtandao mkubwa kuliko taasisi yeyote nchini, na hiyo ndio moja ya siri za uimara wa CCM.


Akizungumzia swala la maadili Nape alidai kuwa CCM ndio chama duniani chenye nyaraka nyingi na bora zinazozungumzia maadili ya viongozi. Pamoja na nyaraka hizo alisema mfumo wa uchujaji majina hasa kwa nafasi ya urais kupitia CCM hautoi nafasi kwa mgombea yeyote wa nafasi hiyo kupita kwa kununua uteuzi huo.


Alisema Nape kuwa wasaka urais wanaohangaika kutoa pesa zao kujaribu kununua uteuzi wa CCM wanapoteza muda na pesa zao kwani Chama hicho hakitawateua kugombea nafasi hiyo.


Nape akatumia nafasi hiyo kuwaomba wachungaji hao kukiombea Chama hicho na viongozi wake wawe na ujasiri wa kulisimamia hilo kwani kupitisha wagombea walionunua uteuzi huo ni kukaribisha laana kwa nchi.


" Nawahakikishia kuwa hakuna mnunua urais atakayepenya mchujo ndani ya CCM. Kuruhusu mtu wa namna hiyo kupenya ni kuleta laana kwa nchi yetu,hivyo viongozi wa dini tuombeeni tuwe na ujasiri wa kutosha kukataa laana hii" alisisitiza Nape.


Nape alisema mwanzoni mwa mwaka huu wa 2015 Katibu Mkuu wa CCM  Ndg. Kinana akitoa salaam za mwaka mpya za CCM mjini Tanga, aliwaambia Watanzania kuwa CCM imekuwa ikisimamia maadili kwa miaka yote lakini mwaka huu itaongeza ukali ili kuhakikisha nchi inapata viongozi waadilifu watakaoisaidia nchi kupiga hatua zaidi.


Anasema Nape hakuna atakayeingia madarakani kwa rushwa atakayeunda serikali itakayokusanya kodi. Bila kukusanya kodi hakuna namna nchi itapiga hatua ya maendeleo na huduma za kijamii zitadumaa na hivyo kusababisha maisha magumu na hiyo itakuwa laana kwa nchi.


Semina hiyo inayofanyika Kibaha mkoani Pwani itahitimishwa tarehe 24/01/2015 na imehusisha wachungaji wa huduma ya Efatha nchi nzima, na baadhi ya wachungaji kutoka nchini Kenya.

HABARI KAIKA PICHA

 MTUME na Nabii wa Kanisa la EFATHA Josephat Mwingira akimlaki kwa furaha, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alipowasili katika ukumbini, kutoa mada kuhusu nafasi ya CCM na uhusiano wa CCM katika jamii, kwnye semina ya wachungaji wa kanisa hilo wa ndani na nje ya Tanzania, inayoendelea Kibahaka mkoa wa Pwani. Watatu kulia ni Mama Eliakunda Mwingira.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akitoa mada kwenye semina hiyo
 Nape akifafanua jambokuhusu CCM ilivyo imara licha ya kuwa na mapungufu kama Taasisi kubwa
 "Hili Chama ni kubwa sana, siyo rahisi kuling'oa madarakani, ukiona unakereka a mambo ingia humohumo ndai ya Chama ukisafishe... hiyo ndiyo dawa", akisema Nape kwenye Semina hiyo
 "Hatukatai kwamba CCM haina mapungufu, inayo lakini mifumo yake ni mizuri kuliko Chama chochote Afrika na pengine duniani kote", alisema Nape kweny Semina hiyo.
 Nabii Mwingira na Mkewe wakimsikiliza Nape kwa makini wakati akitiririka kwenye utoaji mada kwenye semina hiyo
 Washiriki katika semina wakifuatilia kwa makini wakati Nape akitoa mada kwenye semina hiyo
 "Katiba hii ya CCM imesheheni kila kitu.. tatizo ni baadhi ya watu kusuasua katika kuyatekeleza" anasema Nape.
 Nape akimaliza kutoa mada yake kwa kuwaomba watanzania kuhakikisha nchi inapata mgombea wa Urais aliye bora na siyo kwenye kuinunua nafasi hiyo muhimu
 Nape akirejea kuketi baada ya kutoa mada kwa zaidi ya saa moja na nusu kwenye semina hiyo
 Washiriki wakimshangilia Nape baada ya mada yake
 Nape akijibu maswali yaliyoulizwa na washiriki baada ya kutoa mada yake
 Mtume na Nabii Mwingira akitoa maelezo kusadifu maneno aliyotoa Nape katika mada yake.

 Waumini wakiombea Tanzania, CCM na Nape kudumu katika mwendendo ulio bora kwa manufaa ya Taifa la Tanzania
 Nape akiwa amesimama wakati wa maombi hayo
 Nape akienda kukutana na Mwingira kwa ajili ya kuagana baada ya semina
 "Kijana umetoa mada nzuri, Mungu amekuonyesha njia, umezungumza na kujibu maswali vema" Mwingira akimwambia Nape wakati akimsindikiza ktoka ukumbini
 Mtume na Nabii Mwingira akimsindikiza Nape huku wakionyesha kuwa wenye furaha kwa tukio lililotokea la CCM kushiriki kutoa mada kwenye semina hiyo
 Mwingira akimsindikiza Nape hadi nje ya ukumbi
 Mwingira na Nape wakiingia jengo la Utawala la EFATHA, kwa ajili ya kuagana rasmi. 
                 

Rais Dk.Shein Awaalika Chakula Madaktari Bingwa kutoka Uingereza.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein (kushoto) akiwa na madakatari Bingwa wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo  kutoka Uingereza alipowaalika chakula cha mchana Ikulu Mjini Zanzibar leo madaktari hao wapo nchini baada ya kuhudhria mkutano maalum uliofanyika juzi katika Hoteli ya Breezes Hotel Bwejuu Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja,
Baadhi ya Madaktari Bingwa wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo  kutoka Uingereza wakiwa katika  chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein Ikulu Mjini Zanzibar leo, madaktari hao wapo nchini baada ya kuhudhria mkutano maalum uliofanyika juzi katika Hoteli ya Breezes Hotel Bwejuu Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein (kushoto) akiagana na  madakatari Bingwa wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo  kutoka Uingereza alipowaalika chakula cha mchana Ikulu Mjini Zanzibar leo, madaktari hao wapo nchini baada ya kuhudhria mkutano maalum uliofanyika juzi katika Hoteli ya Breezes Hotel Bwejuu Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja,
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamaed Shein (katikati) akiwa katika picha na ya pamoja na na madakatari Bingwa wa maradhi yanayohusiana na mfumo wa utoaji wa haja ndogo kutoka Uingereza alipowaalika chakula cha mchana Ikulu Mjini Zanzibar leo,pia wakiwepo Viongozi wengine wa Serikali, madaktari hao wapo nchini baada ya kuhudhria mkutano maalum uliofanyika juzi katika Hoteli ya Breezes Hotel Bwejuu Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja(Picha na Ikulu)
Askali Polisi, akijaribu  kumuokoa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kigogo Freshi (B) Pugu, nje kidogo ya jijini Dar es Salaam (CCM), Mariana Aruna asipigwe baada ya kutaka kuapishwa kinyume na sheria leo huku akiwa amechaniwa shati
Askali Polisi, akijaribu  kumuokoa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kigogo Freshi (B) Pugu, nje kidogo ya jijini Dar es Salaam (CCM), Mariana Aruna asipigwe baada ya kutaka kuapishwa kinyume na sheria leo huku akiwa amechaniwa shati

Richa:Mwanashelia wa Manispaa ya Ilala, Hela Mlimanazi akiwaapisha Wenyeviti wateule, Japhet Kembo - Chadema Mtaa wa Migombani Segerea na, Mbaya Saleh wa Migombani Kata ya Minazi Milefu Kiwalani

Mwanashelia wa Manispaa ya Ilala, Hela Mlimanazi (kushoto) akiwaapisha Wenyeviti wateule, Japhet Kembo (kulia) Chadema Mtaa wa Migombani Segerea na, Mbaya Saleh wa Migombani Kata ya Minazi Milefu Kiwalani wakati wa hafla iliyofanyika Ofisi za Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam

Tuesday, January 20, 2015


Wolper awachana wasanii wa BongoMovie awaita masnitch, awapa ushauri huu…. SSOma hapa

Kumekuepo na makundi natetesi za kutopendana kati ya wasanii wa Bongo Movie, mara nyingi tumeona wakirushiana maneno na hata mabifu yao kuandikwa na magazeti mbalimbali. Leo kupitia akaunti yake ya Instagram Star Jackline Wolper ameamua kufunguka uozo uliomo kati ya mastar wengi wa Bongo Movie.
wolper
Wolper aliandika ” Nawapenda sana Bongo Movie lakn chakusikitika vile vichwa mnavyoviamin kwenye tasinia ndo masnch wakubwa simtoke huko tafuteni kAzi nyingne km amjasoma kma mm jifunzeni kushona nguo kma mm me sahv na fund wangu mgece naingia class asubuh najion nimeshachoka kutumikishwa na Wahnd ..kipaji changu kingne mitindo so najisogeza kwenye mitindo Mbali mbali syo kubanana sehem ambapo ampendani kazi majungu nakusnchiana kila sku .. Nawahnd awatetereki Maana hao Mnaowaita magwiji ndomsatar wambele kukandamiza .. sasa sjui lengo nn kupata wao tuu au basi tuu roho mbaya..Nikipata Majina yao yote nitawawek na Mapicha yao..siongei kma movie star Naongea kma Mwananch nayependa snaa iliyonishinda nakujitoa bila Matangazo..i hate u wanyonyaji nawachukia saaaaana
Kilichowashtua wengi na kauli yake kua ameamua kuachana na BongoMovie na kuamua kujiingiza katika Fani ya ubunifu wa mavazi. Baadhi ya mashabiki zake waliamua kutoa maoni haya
mwaneywolperfamily1Usitoke mah wengine ndio tunafata nyayo zko kwa kuigiza ss ukitoka mah utatuumiza ss mashabiki zko.Mungu yupo na hyo yote yatakwisha.
gasnizzoTatizo lenu nyinyi mna angariana wenyewe then m1 akichwa kuangaliwa ana lalamika km ww mbona cc wasanii wadogo tushazoea na ndo maana uwa2na sema lazima upitie kwenye msoto kwan we ushawai kuckia msanii mkubwa anakwambia mim niko kwenye msoto yeye anasema nilipita kwenye msoto sasa lin nae msanii mdogo nae atausaau msoto bila ya kufikia kwenye ustar onyesheni ushilikiano ata kwa m2 wachin ww angalia ata mtandaon mnaubaguz uwez kukuta msanii mkubwa kacomments au kaweka like kwa m2 wa chin labda ndugu yake ila cc ndo uwa tunajishaua kwenu maana me sioni km huo ni usilikiano zaidi ya kujishaua yani kila cku ccndo 2we wa2 wakujishusha kwenu badilikeni sisi sote sawa we jiulize mfano misiba mingapi ya wasanii imepita ma katika hiyo micba kati ya wasanii na mashabiki nani wanakuwaga wengi yani bado 2 amjifunzi na uwez kukuta wasanii wanaenda kwenye msiba wa m2 ambae ayupo katka tasnia yao so ili ni somo mcnichukie kesho mkaninyima kaz me niko free kwa kila m2!!!!!!!!!

FID Q kama aliyajua Maamuzi ya Nikki Mbishi akawa kama anamshauri kwenye Siri ya mchezo

fid q
Baada ya habari ya kushtua ya msanii wa Hip hop NIKKI MBISHI,kutangaza kuacha MUZIKI.
Leo nakuletea baadhi ya mistari ambayo msanii mwenzake wa hip hop ambaye kwa kiasi kikubwa alimu_Inspire ni kama aliyaona haya.
Mstari wa kwanza “Alete Bingo mshiko star aishi simple, Sanaa iko hivyo sometimes hukataa kukaa ulipo”
Hapa alijaribu kuelezea kuhusiana na kukosa HELA licha ya kufanya Muziki akisisitiza kuna muda sanaa inaweza kukukataa.
Akaendelea
“wanaodharau hujiletea matatizo hawajui kwamba wadau hupendelea kukuona hivyo, BONGE la star DONGE la njaa hauna KITU.”
Hakuna ubishi Kuwa jina la NIKKI MBISHI ni jina kubwa sana kwenye game ila “How much The game Pay Him” ndo tunarudi kwa FID Q BONGE la Star DONGE la Njaa HAUNA KITU.
FID Q pia ni kama alitoa ushauri kwa NIKKI MBISHI kwa kusema “Ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa,”- kuacha game kwa Nikki huenda alishindwa tu kujiandaa na FID Q Alisema ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa.
Anaendea baada ya ukishindwa kujiandaa jiandae kushindwa “Mjinga utaachwa unashangaa kumuona Martin Kandinda, Usmart anaoutinga, majumba mandinga ya bwana ALMASI je hizi track za harakati ni UJINGA??
Nadhani alitumia mfano wa Martin kadinda ila in actual manner alimaanisha Wasanii wanaong’aa (Bongo Fleva Artist) na neno ALMAS kwa martin kadinda alimaanisha DIAMOND platnums, ambayo kiusanii ni hawa maboss wanaotajwa tajwa kwenye nyimbo, mameneja wa wasanii wanaofanya wasanii wang’ae. Mwishoni mwa huo mstari FID Q alihoji “je hizi track za harakati ni UJINGA? akimaanisha hip hop. Maana wao hawana hao kina ALMAS wa Martin Kadinda..
Akaendelea kwa kusema “Nguvu ya mamba ni maji ,na umaarufu au KUTAMBA kushika namba ni BAHATI/”
Huu mstari nao pia ni kama ushauri na kutia moyo kuwa sometimes kuwika ni bahati tu,kwani wasanii wangapi ni wabovu kabisa ila ni mastar wakubwa kwa huohuo ubovu wao.

Hebu tuambie unaipenda couple ipi kati ya Chibu na Zari na Vannesa Mdee na Jux??

DIMONDDDDDE
Vee Mtonyo na Jux

mahaba nitetemesheeee kama umemeee


Zee n Mondi
Kohokohooooo, leo ni mambo ya maloveeee, couple ipi kati ya hizo mbili unayoipenda?? naomba kama kuna nyingine unazozijua za uhakika please ututajie ila si za uzushi, kuna watu wameniomba niandike hii ila wakaongeza ya Kajala na Quick Rocka ila kwakuwa sijathibitisha sija add hapo, haya na wewe unaweza ukatoa mawazo kama una couple unayoijua nzuri, kama huna jimwage kati ya hizo mbili…… ipi nzuri???  watu na ma baby zao wenye vifua haswa sio kifua mosquito chest kama wewe ndo wa mosquito chest usionee wenzio wivu kitulize kama mabaga fresh….

Wasanii Ambao Hata Watoe Nyimbo Unajua tu Hamna Kipya, Sauti na Melody zile zile

sharobobjunior
1.Roma Mkatoliki,..beats zake karibia zote sawa,nyimbo zake zote ujumbe sawa(harakati)
2.Izzo Bizness yaanii huyu beats zinafanana kila wimbo,mfano chorus ya wimbo mmoja unaweza kuimbia nyimbo zake
zote bila tabu.
3.AY,huyu ndo hana kipya style ile ile,mfano video ya leo na nyimbo baada ya hapo kitu kile kile hamna kipya.
4.Tuda man,huyu hata huwezi kujua analia au anaimba,iwe wimbo wa starehe kama analia tu.
5.Stamina (huyu atachokwa mda si mrefu anadhani misamiati ndo kuwashika watu
6.Young Killer asipoimba bongo fleva hatadumu.
7.Linex nyimbo zake hamna tofauti,kinachomfanya asikike ujumbe wa nyimbo zake.
8.Ben Pol huyu naye hana kipya
9. Jaquar wa Kenya Naye Balaa Nyimbo zake zote zinafanana
10. Bob Junior Mzee wa Kulia kulia kila nyimbo
Toa mawazo yako na ikiwezekana ongeza list 

Monday, January 19, 2015


Msanii anayefanya vizuri kunako kiwanda cha filamu Bongo, Wastara Juma.
MSANII anayefanya vizuri kunako kiwanda cha filamu Bongo, Wastara Juma amefunguka kwamba tasnia ya filamu kwa sasa inaonekana kama imeingiliwa na pepo mbaya kutokana na mambo kwenda ndivyo sivyo kila kukicha.

 Akizungumza na gazeti hili, Wastara alisema tasnia ya filamu imekuwa ni ya migogoro, chuki huku bei ikishuka  jambo ambalo siyo sahihi kwani litawarudisha nyuma wasanii wakati hata kazi hiyo hailipi kihivyo. 

“Mimi sitengenezi filamu mpaka nielewane na bosi bei kabisa lakini vinginevyo ndiyo maana nimeamua kujikita kwenye biashara ili niweze kuendeleza maisha ya kila siku maana tasnia haieleweki sasa hivi, naona kama pepo mbaya ametuvamia inatakiwa tumuombe Mungu sana,” alisema Wastara.