LORI LA MAFUTA LAUA NA KUJERUHI TENA MBEYA
WATU WAWILI 1. MARIA PAJELA [18] NA 2. WILLIAM S/O PASCHAL [38] ,WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IDWELI, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA, WALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUUNGUA MOTO KIJIJINI HAPO JANA.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI LEO, IMESEMA KUWA, KATIKA
TUKIO HILO MAREHEMU HAO PAMOJA NA BAADHI
YA WANANCHI WENGINE WA KIJIJI HICHO WALIKUWA KATIKA HARAKATI ZA KUIBA
MAFUTA KUTOKA KATIKA GARI T.891 AQZ /T.821 ARF AINA YA SCANIA MALI YA AILIS SANGA LILILOKUWA LIMEBEBA MAFUTA
AINA YA PETROLI UJAZO WA LITA 41,000, LIKITOKEA DSM KUELEKEA NCHINI
MALAWI, LIKIENDESHWA NA DEREVA ZAWADI NYATO [46] MKAZI WA SAE MBEYA
AKIWA NA TINGO WAKE FRANK YOHANA
[24],MKAZI WA MBOZI.
AWALI
KABLA YA TUKIO HILO GARI HILO LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA, HIVYO WAHANGA [DEREVA
NA TINGO] WALIFANIKIWA KUOKOLEWA NA KUPELEKWA KITUO CHA POLISI KIWIRA ILI
KUPATA HATI YA MATIBABU [PF3] KWA AJILI YA KWENDA HOSPITALINI KUPATIWA MATIBABU.
HATA HIVYO BAADHI YA WANANCHI WA ENEO HILO WALIVAMIA GARI HILO NA KUFANIKIWA
KUTOBOA TANKI LA MAFUTA, HALI ILIYOPELEKEA MAFUTA KUANZA KUMWAGIKA/KUSAMBAA
MAENEO HAYO NA HATA KUELEKEA MAENEO YENYE MAKAZI YA WATU NA WAO KUKINGA KWA KUTUMIA VYOMBO VYAO.
KATIKA
TUKIO HILO WATU KUMI NA NANE [18] WALIJERUHIWA, KATI YAO WANAUME NI 13 NA
WANAWAKE 05 AMBAO NI: 1. SHUKURU KANZALE [21], 2. NURU GEORGE [30], 3.ASANTE
BONIFACE [38], 4. JOSEPH JAMSON [18], 5.JOSEPH PASCHAL [30], 6.SIZA KANESA
[22], 7.ALEX DAUD [35], 8. OSCAR YOSIA
[23], 9.TRAIPHON MOASI [37], 10.SAMSON MBWILA [29].
WENGINE NI 11. DORA MICHAEL [35],12. VERONICA ELIA [30],13.RABSEN AYUB [26], 14.WASIWASI SPIKA [32], 15.ASIA ANON [20], 16.BAHATI KYANDO [23], 17. CHRISTOPHER ERASTO [32] NA 18. MELISA SANANE [50], WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IDWELI. AIDHA KATI YA MAJERUHI HAO,MAJERUHI 16 WAMELAZWA HOSPITALI YA MISHENI –IGOGWE NA MAJERUHI WAWILI WAMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA-TUKUYU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.
Wednesday, February 18, 2015
Wapiganaji 300 wa Boko Haram wauawa
jeshi la Nigeria limesema kuwa
limewauwa zaidi ya wapiganaji 300 wa Boko Haram, baada ya jeshi la nchi
hiyo kutwaa tena miji kadhaa iliyotekwa na wapiganaji hao kazkazini
mashariki mwa Monguno.
Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.
Siku ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi uliopita.
Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji wachache wa kiislamu pia wamekamatwa.Bado hakujatolewa taarifa zaidi kuthibitisha habari hizo.
Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.
Siku ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi uliopita.
No comments:
Post a Comment