Tuesday, February 10, 2015

JB KUTOKA NA MZEE WA SWAGA

Jacob Stephen
Filamu ya Mzee wa Swaga.
BAADA ya filamu yake ya Mikono Salama kutesa katika soko la filamu Swahilihood sasa gwiji wa filamu Jacob Stephen ‘JB’ anakuja na filamu kali na ya kusisimua ya Mzee wa Swaga akiwashirikisha wasanii wakali katika tasnia ya filamu ya Bongo.

Cassie Kabwita, wastara juma, ndumbagwe Misayo
Wasanii walioshiriki katika filamu ya Mzee wa Swaga
Jacob Stephen
Jb akiwa katika pozi la picha
Filamu ya Mzee wa Swaga
Filamu ya Mzee wa Swaga
Wellu Sengo, Jacob Stephen
Jb akiwa na Wellu Sengo katika moja ya scene za filamu
Wasanii walioshiriki katika filamu hiyo ni Wastara Juma ‘Stara’, Ndumbagwe Misayo ‘Thea’, Wellu Sengo, Cassie Kabwita kutoka nchini Zambia, Nassor Ally, na wasanii wakali kutoka Bongo Movie wameshiriki na kuonyesha uwezo wao.
Mzee wa Swaga inatarajia kutoka wiki hii siku ya Alhamis na kusambazwa katika maduka yoyote ya kuuza filamu Bongo ni kazi iliyotengenezwa katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Zanzibar na Dar es Salaam kuifanya iwe tofauti na sinema nyingine ambazo zinatengenezwa na kampuni za filamu.

No comments:

Post a Comment