CASSIE KABWITA ATAMBA KUIGIZA BONGO
MWIGIZAJI wa kike wa filamu kutoka Zambia Cassie Kabwita ametamba kuwa ana uwezo katika uigizaji na ndio sababu ambayo imemfanya aweze kuitwa na kushiriki katika filamu kubwa nchini na anaamini kuwa kasi aliyo nayo anaweza kuwa kinara katika sinema za Bongo.“Naipenda Tanzania inafanya vizuri katika sinema na najikubali kuwa ni msanii mzuri kuweza kuigiza na msanii mkubwa kama Jacob Stephen ‘Jb’ ni hatua nzuri first time nilicheza katika sinema ya Vita baridi pia nimecheza sinema ya Mzee wa Swaga,”
Cassie anafurahia kushirikiana na wasanii nyota kama Thea, Wastara ambao aliweza kuigiza nao kukubali uwezo wao wa kuigiza lakini anajivunia kuchaguliwa kama msanii pekee kutoka Zambia na anaamini anawakilisha nchi yake vema msanii sinema aliyoshiriki ya Mzee wa Swaga imetoka mwaka huu chini ya JB.
No comments:
Post a Comment