Mez B afariki dunia asubuhi ya leo, dada na kaka yake wathibitisha
Msanii wa Bongo fleva aliekuwa anaunda kundi la Chemba Squard, Moses
a.k.a Mez B amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa nyumbani kwao Dodoma
baada ya kuugua kwa muda.
kutokana na kauli ya dada yake mzazi na mdogo wake wa kiume, Mez b
ameugua kwa wiki nne mfululizo, alishalazwa takribani mara nne na "kila
mara alikuwa akipata nafuu na kurudi nyumbani, lakini leo hii amezidiwa
ghafla na ndio akafari." amesema dada wa Mez b.
"Naitwa Recho dada ake na Mez b, amefariki dunia leo
asubuhi, kwasasa yupo hospitali, alikuwa anaumwa , alikuwa ana homa na
pia alikuwa na tatizo la kuishiwa damu, kwa leo hakuwa amelazwa lakini
tulimpeleka baada ya kuwa hali imebadilika, alilazwa wiki iliyopita
kwahiyo alipopata nafuu akawa amerudishwa nyumbani, lakini jana alikuwa
ok na tukakuta asubuhi alikuwa ok, lakini ilipofika mida ya saa nne hali
ikabadilika ndio akafariki, yupo hospitali ya general."
No comments:
Post a Comment