Friday, February 27, 2015

Matukio mbalimbali ya ziara ya Waziri Mkuu Pinda Mbeya mjini na vijijini

PG4A2882
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wananchi baada ya kufungua vyumba vitatu vya Maabara katika shule ya sekondari ya Songwe mkoani Mbeya Febrari 25, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
PG4A2919
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwasikiliza wanafunzi wa shule ya sekondari ya Iwambe wilayani Mbeya wakati alipofungua na kukagua maabara tatu za shule hiyo akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari 25, 2015. Wapili kushoto ni mkewe Tunu na Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Norman Sigalla.
PG4A2988
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua soko Kuu la Mjini Mbeya la Mwanjelwa baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wake akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya, Februari 25, 2015.
PG4A3031
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwapungia wananchi wa Kijiji cha Kimondo, Mbeya Vijijini  kabla ya kuweka jiwe la Msingi la zahanati yao akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya Februari 25, 2015. Kushoto kwake ni Mbunge wa Mbeya Vijijini, Luckson Mwanjale na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mbeya mjini Dr. Norman Sigalla.
PG4A3034
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiweka jiwe la Msingi la zahanati ya Kimondo , Mbeya Vijijini akiwa katika ziara ya mkoa  wa Mbeya, Februari 25, 2015. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mjini Dr. Norman Sigalla.
PG4A3046
Waziri Mkuu, Mizengo PInda akizungumza na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Zahanati  ya Kimondo, Mbeya Vijijini  akiwa katika ziara ya mkoa wa huo, Februari 25, 2015.
PG4A3074
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akisalimiana na wananchi baada ya kuweka jiwe la msingi la Zahanati ya Kimondo na kuzungumza akiwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya, Februari 25, 2015.
PG4A3106
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia Mkutano wa hadhara katika kijiji cha Igoma , Mbeya Vijijini akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya Februari 25, 2015.
PG4A3137
Wasanii, Max Oswald (kushoto) na  Ivan Kina wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara  uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kijiji cha Igoma, Mbeya Vijijini Februari 25, 2015.

Thursday, February 26, 2015

Breaking News: Chid Benz Ahukumiwa Kifungo cha Miaka Miwili Jela au Kulipa Faini ya sh. 900,000


Mwanamuziki wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Rashidi Abdallah Makwaro Maarufu kama (Chid Benzi) amehukumiwa kifungo cha miaka mwili jela au kulipa faini ya shingili laki tisa bada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ikiwemo kukutwa na dawa za kulevya aina ya heroin yenye thamani ya sh. 38,638, bangi ya sh. 1,720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo kijiko na kigae.

Chid Benz alikamatwa mwaka jana katika Uwanja wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam akiwa na madawa hayo.
 
Mwanamuziki huyo ambaye alikiri kosa hilo wiki iliyopita, alikamatwa uwanjani hapo akiwa anajitayarisha kupanda ndege kwenda Mbeya kwenye tamasha la muziki.

Hata  hivyo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo   imemwachia  huru mwanamuziki huyo  baada ya kulipa faini ya 900,000/

Tuesday, February 24, 2015

Diamond atoa sababu za kushindwa kuhudhuria mazishi ya baba wa Dully Sykes

Baada ya kutupiwa shutuma na lawama nyingi kupitia mitandao ya kijaa kwa sababu ya kutokuweza kuhudhuria msiba wa marehem baba wa swahiba wake na kaka yake (kama anavyomuita) Dully Sykes, Mzee Abby Sykes huku akionekana akila bata na mpenzi wake Zari zanzibar, Diamond aamua kufunguka upande wake na sababu za kushindwa kufika katika mazishi.
Diamond amesema msiangalie mnachokiona katika Instagram mkajua mtu labda alikuwa anafanya starehe.....


"watu tu waliniona niko zanzibar, lakini ukweli hwajua zanzibar nmeenda kufanya nini, usiangalie kila unachokiona kwenye instagramukajua mtu labda kwasabbu alikuwa anafanya starehe, niko katika kipindi ambacho sio kizuri kwangu mimi, kwangu na kwa familia yangu, kwasababu kuna vitu ambavyo siwezi kuvizungumza, lakini, na siwezi kuweka kwenye media ndio maana watu wengine wanaweza kuniana nacheka nafanya nini, lakini nipo katika situation ambayo, kwanza mama yangu anaumwa sana sijawahi kulizungumza hilo nalizungumza hapa, hapa ninavyoongea na wewe yupo India, so kuna vitu vingi vinaendelea siwezi kusema nilikuwa zanzibar nafanya nini, inawezekana ikawa ndio sababu imenifanya mpaka mimi nikachelewa kwenda kwenye msiba....unajua wakati mwingine ni vizuri kwenda kuzika lakini inawezeka mtu akawa ameenda kuzika lakini mimi nikawa sijaenda kuzika nikawa nimefanya cha maana kuliko alieenda kuzika kwasabau huwezi kujua nimefanya kitu gani.so watu hawakawii kuongea niliskia naambiwa mimi sijui Diamond hajafika lakini naamini watu wengi hawakufika na kila mtu hakufika kwasababu flani.mi sio mpuuzi, kwasababu mimi na Dully ni kama, dully mi ni kama kaka yangu kabisa, ni mtu ambae amenisaidia vitu vingi sana, isingewekana kabisa mi niko na nina nafasi nishindwe kwenda kwenye msiba, ukiacha tu dully lakini mtu aliefariki ni kama mzee wangu na ni mtu ambae amefanya vitu vizuri  amefanya kitu kikubwa katika sanaa hii ya mziki na mi nimefika hapa yeye pia ana mchango wake, so haikuwa rahisi eti mi nisiende tu eti nikiwa sina sababu, kulikuwa sababu na ndio maana." alimaliza kwa kusema Diamond.

Mez B afariki dunia asubuhi ya leo, dada na kaka yake wathibitisha

Msanii wa Bongo fleva aliekuwa anaunda kundi la Chemba Squard, Moses a.k.a Mez B amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa nyumbani kwao Dodoma baada ya kuugua kwa muda.
kutokana na kauli ya dada yake mzazi na mdogo wake wa kiume, Mez b ameugua kwa wiki nne mfululizo, alishalazwa takribani mara nne na "kila mara alikuwa akipata nafuu na kurudi nyumbani, lakini leo hii amezidiwa ghafla na ndio akafari." amesema dada wa Mez b.
"Naitwa Recho dada ake na Mez b, amefariki dunia leo asubuhi, kwasasa yupo hospitali, alikuwa anaumwa , alikuwa ana homa na pia alikuwa na tatizo la kuishiwa damu, kwa leo hakuwa amelazwa lakini tulimpeleka baada ya kuwa hali imebadilika, alilazwa wiki iliyopita kwahiyo alipopata nafuu akawa amerudishwa nyumbani, lakini jana alikuwa ok na tukakuta asubuhi alikuwa ok, lakini ilipofika mida ya saa nne hali ikabadilika ndio akafariki, yupo hospitali ya general."

Pheeeeew!! Hatimae Floyd Mayweather atangaza siku ya mpambano kati yake na Manny Pacquiao

Baada ya miaka kibao ya kukubaliana, hatimae Floyd Mayweather amekubali kuingia ulingoni na mfilipino Manny Paquiao tarehe 2 mwezi watano MGM Grand, Las Vegas.
“Niliwaahidi mashabiki wangu tutafikia muafaka na tumefikiaI,” amesema Mayweather jana (ijumaa) “tutatengeneza history tare 2. msikose.”
Mayweather ametangaza baada ya wiki kadhaa za maelewano na fununu za kama ngumi kati ya unbeaten Mayweather na eight-division champion Pacquiao zitafanyika.
mara ya kwanza walijaribu kukutana mwaka 2010, lakini mazungumzo yaliishia kati baada juu ya utaratibu wa upimaji wa madawa ya kulevya.Tangu siku hiyo kila jaribio kuwakutanisha ulingoni wawili hao liligonga mwamba kutokana na sababu mbali mbali.
lakini majadiliano yakawa kweli baada ya Pacquiao kumtandika Chris Algieri mews November mwaka jana katika mapigano yaliyofanyika Macau, na kisha kum-challenge hadharani Mayweather ulingoni.
“nimefurahi sana chamber Mayweather na mimi kuwapa mashabiki mpambano walioutaka kwa miaka mingi,” amesema Pacquiao. “Wamesubiri vya kutosha na wanastahili.”
Mazungumzo yalikuwa na utata kutokana na ukweli kuwa Mayweather ana mkataba wa kipekee na Showtime, wakati HBO wana haki na Pacquiao. Mitandao hiyo miwili imefikia maelewano kwa uhakika wa kufanya mkutano wa wito pamoja siku ya ijumaa.
Kila mtu anaehusika, wakiwemo Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wanajua mpambano huu ilikuwa utokee," Amesema Meneja mkuu wa Showtime, Stephen Espinoza. "Sote tumefurahi kuwa na uwezo kuwaleteeni tukio hili kwa mshabiki wa ndondi duniani kote."
Ken Hershman wa HBO alisema: " Manny Pacquiao na Floyd Mayweather wamekuwa wapiganaji maarufu katika mchezo wa ndondi kwa muongo mmoja uliopita na mashabikiwa ndondi duniani kote wamekuwa wakitaka kwa hamu wawili hao kukutana ulingoni. Sasa Mei 2 kila mtu anaamini itakuwa ni tukio kubwa la ndondikuwahi kutokea, mashabiki wa ndondi wapewa walichukuwa wakikiomba. Mei 2 itakuwa ni wakati sahihi kwa ajili ya mchezo wa ngumi na HBO Sports ina furaha kubwa kuwa sehemu ya tukio hili la kuvutia. "
Mpambano huo unadhaniwa kuwa mpambano tajiri katika historia ya ndondi. Unategemewa kuwa wa kishindani na kuwa na thamani ya kulipa $ 100 kwa ajili ya kulipa -kwa- mtazamo , ingawa Espinoza alisema bei Play Per Viw (PPV) "bado haijaamuliwa." Inategemewa utakwenda kimataifa na kuchukua ndondi mainstream.

Taarifa Rasmi ya Jeshi la Polisi Kuhusiana na Sakata la Kutekwa kwa Wanajeshi wa JKT Waliotaka kuandamana Kudai Ajira



Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam linawashikilia vijana watano wa kundi la wahitimu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa tuhuma za kufanya uchochezi na kufanya mikusanyiko isiyo halali jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema vijana hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti kwa makosa ya kuunda kikundi kisicho halali kwa mujibu wa sheria za nchi na kuwahamasisha wenzao, kuandamana hadi Ikulu kwa Rais Jakaya Kikwete kudai ajira za kudumu.
 
“Tunawashikilia vijana watano ambao ndio viongozi wa kikundi kinachojiita umoja wa wahitimu wa Jeshi la Kujenga Taifa. Mwenyekiti ndio alikuwa wa kwanza kukamatwa na wengine tuliwakamata juzi mara baada ya kukusanyika eneo la Msimbazi Centre na Muhimbili,” alisema Kova.
 
Akieleza chanzo cha vijana hao kutaka kuandamana kuelekea Ikulu, alidai wahitimu hao wanadai kuahidiwa ajira za kudumu walipomaliza mafunzo yao na hivyo baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kuajiriwa, ndipo wakaamua kuanzisha kikundi hicho ili kwenda kumwona Rais  Kikwete kumweleza tatizo la ajira linalowakabili.
 
“Vijana hawa wanadai kuwa waliahidiwa kupewa ajira za kudumu mara baada ya kumaliza mafunzo yao ya JKT.
 
" Jambo hili sio la kweli, kwani tumefanya uchunguzi na kubaini hakuna mkataba wowote unaosema wakimaliza mafunzo lazima waajiriwe, bali kila mtu anatakiwa kutumia ujuzi alioupata kujiajiri.  
 
"Lakini walipokaa kwa muda mrefu  bila kuona ahadi yao inatekelezwa, wakaamua kuanzisha kikundi chao ambacho sio halali kwa mujibu wa sheria za nchi.
 
"Hadi sasa tumeandaa jalada la mashitaka na tumelikabidhi kwa mwanasheria wa serikali kwa ajili ya kuwafikisha mahakamani watuhumiwa hawa kujibu mashitaka yanayowakabili,” aliongeza Kova katika taarifa yake.
 
Alitaja vijana wanaoshikiliwa na Polisi kuwa ni Mwenyekiti wa kikundi hicho George Mgoba (28) mkazi wa Mabibo Loyola, Katibu wao Linus Emmanuel (28) mkazi wa Tabata, Emmanuel Richard (28) mkazi wa Kawe, Jacob Joseph (36) mkazi wa Mabibo na Rizione Ngowi (27) mkazi wa Mtoni Mtongani.
 
Akizungumzia tuhuma za kutekwa na kuteswa kwa George Mgoba, Kova alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ili kubaini tukio hilo kama ni la kweli na kwanini watu hao walimteka.
 
 “Tunaendelea na uchunguzi kubaini kama ni kweli kijana huyo alitekwa kama anavyodai kuwa Februari 16 alitekwa na kupatikana tarehe 19 majira ya saa  nne usiku huko Tungi Kibaha kandokando ya barabara, pia tujue ni akina nani walimteka na kwasababu zipi kisha watu hao tutawapeleka mahakamani,” alisema Kova.
 
Kova alieleza kuwa “Februari 22 mwaka huu majira ya saa kumi na moja jioni, George Mgoba alijaribu kutoroka wadini katika Hospitali ya Muhimbili lakini polisi walibaini ujanja wake na kufanikiwa kumweka kizuizini. Lengo lake ilikuwa ni kukimbia matibabu na kuzua hofu kwa wananchi”.
 
Kwa sasa Mwenyekiti huyo wa vijana hao bado amelazwa katika  Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, akipatiwa matibabu. 
 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja katika Hospitali  hiyo ya Muhimbili, Aminiel Aligaesha  alisema jana kuwa hali ya mtu huyo, inaendelea vizuri na afya yake imeimarika.
 
Wakati huo huo, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari baadaye jana, Kova alimtaka Makamu Mwenyekiti wa Vijana hao, Parali Kiwango (25) mkazi wa Temeke Mikoroshini ajisalimishe mara moja Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi, kabla jeshi hilo halijaanza kumtafuta.
 
“Jeshi la Polisi linamtaka Makamu Mwenyekiti ajisalimishe mara moja kwani jana alipoona Katibu wake amekamatwa alikimbia na kutokomea kusikojulikana. 
 
"Yeye kama ni mhitimu wa JKT hatakiwi kukimbia, bali ajisalimishe mwenyewe katika ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Polisi Kanda  Maalumu Dar es Salaam au kituo chochote cha Polisi kilicho karibu na alipo,” aliongeza Kova. posted by  dayana mchina kilima

NACTE YAFUNGUA APPLICATION ZA AFYA CERTIFICATE,DIPLOMA NA DIGRII-SOMA HAPA ILEJE NI NYUMBANI


                                  
Baraza la mitihani nacte limefungua Usajili kwa wanafunzi wanaotaka kusomea afya cheti hadi digrii ambapo kwa mara ya kwanz achuo cha st.josephy chatoa digrii mpya ya clinical medicine miaka minne.

PUBLIC NOTICE - OPENING OF CAS
OPENING OF THE CENTRAL ADMISSION SYSTEM (CAS) FOR NEW APPLICANTS
MARCH INTAKE

The National Council for Technical Education (NACTE) would like to inform the public that Central Admission System (CAS) is now open for new applicants into:
1. Health Training Institutions (Ordinary Diploma and Certificate in Nursing) for  March 2015 intake into  the following institutions,
  • A3 Institute of Professional Studies - Ilala, DSM,
  • Mikocheni Nursing School - Dar es Salaam 
  • Massana College of Nursing - Dar-es-Salaam
  • St. Glory Nursing School- Dar-es-Salaam
  • Ilembula Institute for Health and Allied Science
  • Mbalizi Health Institute
  • Yohana Wavenza Health Institute
  • St. John College of Health Science
  • Isimila Nursing School
  • St. Aggrey College of Health Science
  • Tumaini University Makumiza – Mbeya Campus 
NOTE: All applications should be done online through  and the deadline on this application will be on 13th March 2015.

2. Bachelor of Clinical Medicine for  March 2015 intake at St.Joseph University College of Health and Allied Sciences.
  • Duration: Four (4) years
  • Entry Requirement: Ordinary Diploma in Clinical Medicine (GPA 2.7 or above)
  • School fees: 6,260,400/=
  • Date of Commencement of Program: 20th April, 2015

Monday, February 23, 2015

Mwanajeshi Mwingine wa JKT ambaye ni Katibu wa Vijana wa JTK Waliotaka Kuandamana Akamatwa Akituhumiwa Kufanya Mkusanyiko Usio Halali



KATIBU wa vijana waliopata mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokuwa wakiandamana kushinikiza Serikali kuwapatia ajira, Rinus Emmanuel amekamatwa jijini Dar es Salaam.
 
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wao George Mgoba, kutekwa wiki iliyopita na kisha kupigwa na kuteswa na watu wasiojulikana.
 
Hata hivyo Mgoba alihamishwa kutoka Hospitali ya Amana, Ilala na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ambapo anaendelea kupata mateso kutokana na kutopatiwa matibabu katika hospitali hiyo.
 
Katibu huyo alikamatwa jana akiwa na wenzake wawili wakati wakiwaongoza wenzao kwenda kumwona mwenyekiti wao, aliyelazwa katika Hospitali ya Muhimbili.
 
Akizungumza na Mpekuzi jana, Msemaji wa vijana hao, Omary Bakari alisema katibu wao alichukuliwa ghafla na polisi walipokuwa wanaingia eneo la Muhimbili muda mchache baada ya kushuka kwenye gari.
 
“Hatujui nini kinaendelea hadi sasa na kwa nini polisi wanatufanyia vitendo hivi wakijua sisi si wahalifu, tunasikitika sana kwa haya yanayoendelea kufanyika juu yetu,” alisema Bakari.
 
Alisema pamoja na kukamatawa kwa katibu wao na watu waliodai ni askari polisi wamefuatilia kwa vyombo vinavyohusika ikiwemo polisi lakini wamekuwa wakipewa majibu ya kukatisha tama, jambo ambalo linawafanya waingiwe na hofu kuhusu hatima ya kiongozi wao.
 
Zaidi ya vijana 300 walikuwa wakiingia hopitalini hapo , huku baadhi yao wakiwa nyuma ghafla walishuka askari wakiwa wamevaa kiraia ambao walimvamia katibu wao na kuingia nae katika gari na kutokomea naye kusikojulina.
 
Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa vijana hao, Kiwango Mpalare, alisema kabla ya kwenda Muhimbili walikuwa na kikao chao katika Ukumbi wa Msimbazi Centre ambapo pamoja na mambo mengine walijadili hatima ya kumuuguza kiongozi wao.
 
“Baada ya kikao wote tulitoka na kuazimia kwenda hospitali ya Taifa Muhimbili kwa lengo la kumjulia hali kiongozi wetu.
 
“Baada ya kufika hospitali tukiwa zaidi ya vijana 300 walikuja askari wakiwa katika gari na kumkamata katibu wetu kwa kosa la kukusanyika kinyume cha sheria. Tunajiuliza wapi tumekusanyika hali ya kuwa tulikuwa kwenye ukumbi wa mikutano.
 
“… je hata katika ukumbi wa mikutano napo kunahitajika kibali cha polisi, baada ya taarifa hiyo tulifuatilia polisi na kuambiwa kuwa waende wanasheria kwa ajili ya dhamana. Lakini ilishindika na wote wapo Kituo cha Polisi Cetral,” alisema Maparale.
 
Mwandishi  alipomtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kiliposi Ilala, Mary Nzuki ili kupata ufafanuzi kuhusu kukamatwa kwa vijana hao alipokea simu na alipoulizwa swali aliikata.
 
Hata alipopigiwa kwa mara nyingine zaidi ya mara tatu simu yake iliita bila kupokelewa.
 
Kutokana na tukio hilo alipotafutwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salam, Kamishna Suleiman Kova, alisema bado hajapata taarifa za kukamatwa kwa vijana hao ambapo aliomba afanye uchunguzi wa kina na taarifa atatoa leo.
 
Wiki iliyopita kiongozi wa vijana hao, Mgoba alitekwa na kisha kuteswa na watu ambao hawajajulikana, alihamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili Ijumaa jioni akitokea Hospitali ya Amana alikokuwa amelazwa awali.
 
Mpekuzi  lilifika Muhimbili jana ikiambata na vijana hao hadi  wodi namba sita jengo la Mwaisela na kumkuta Mgoba amelazwa huku akiwa chini ya ulinzi mkali wa polisi ambao walikuwa wamevalia nguo za kiraia.
Mwenyekiti wa JKT, George Mgoba akiwa wodini.
Baadhi ya askari wa JKT wakiwasili Muhimbili.
 Askari  Wakiimarisha  Ulinzi  eneo  la  Hospitali  ya  Muhimbili

Saturday, February 21, 2015

Hii ni ya mwanamke kumkata mpwa wake sehemu zake za siri Ruvuma…

knife-bloodMtu mmoja wa Kijiji cha Majimaji Ruvuma, Patrick Vitus amekatwa sehemu zake za siri  na kuachwa zikining’inia.
Ofisa Mtendaji Wa Kijiji hicho Hussein Mkali amesema Partick alikatwa sehemu zake za siri na mpwa wake Zainabu Saidi baada ya kumkatalia kwenda kumfuata mume wake anayeitwa Musa Said ambaye alikuwa kwa mke mdogo.
Baada ya kufanya tukio hilo Ofisi ya Kijiji ilimkamata Zainabu na kumpeleka katika kituo cha Polisi, huku Patrick akipelekwa Hospitali ya Tunduru kwa ajili ya matibabu.
Chanzo: Gazeti la Mtanzania, Feb 21 2015.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wote.      
                                               by dj dayana kachuchu baby

Kiongozi wa vijana JKT atekwa, aokotwa

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu 

Kwa ufupi
Si Jeshi la Polisi mkoani Pwani wala Dar es Salaam lililokuwa tayari kuzungumzia tukio la kijana huyo kutekwa, kupigwa na kutekelezwa kwenye msitu huo, lakini msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) alithibitisha kuwapo kwa kijana huyo hospitalini hapo kuanzia jana saa 10:30 jioni, ingawa hakutaka kutoa maelezo mengi.
Dar es Salaam. Utata umezingira suala la kijana George Mgoba, ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa kiongozi wa wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) baada ya habari kuwa alitekwa na baadaye kutupwa kwenye Msitu wa Pugu, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Si Jeshi la Polisi mkoani Pwani wala Dar es Salaam lililokuwa tayari kuzungumzia tukio la kijana huyo kutekwa, kupigwa na kutekelezwa kwenye msitu huo, lakini msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) alithibitisha kuwapo kwa kijana huyo hospitalini hapo kuanzia jana saa 10:30 jioni, ingawa hakutaka kutoa maelezo mengi.
Mgoba amekuwa akihamasisha vijana wenzake waliohitimu ya JKT kukusanyika jijini Dar es Salaam na kuandamana hadi kwa Rais ili kumweleza masikitiko yao ya kutopatiwa ajira baada ya kumaliza mafunzo kama walivyoahidiwa wakati wakienda kwenye kambi za jeshi hilo.
“Ndio aliletwa hapa majira ya saa 10:30 akitokea Hospitali ya Amana,” alisema ofisa uhusiano wa MHN, Aminiel Aligaeshi.
“Lakini waganga walipotaka kumtibu alikataa kwa sharti kwamba atibiwe wakati ndugu zake wakiwapo. Ndugu zake walipofuatwa nje, hawakuonekana. Anaonekana ana maumivu sehemu ya mgongoni na anapumua kwa shida.”
Habari zinasema kuwa kuanzia saa 1:00 jioni madaktari walikuwa wakijaribu kumshauri akubali kutibiwa, lakini akakataa na hivyo kuwalazimu madaktari kumtaka asaini fomu ya kukataa matibabu. Hata hivyo hadi saa 2:00 usiku hakuwa amesaini.
Kijana huyo anasemekana kutekwa juzi jioni na watu ambao hawajajulikana na aliokotwa na msamaria mwema ambaye baadaye aliungana na watu wengine kumpeleka Hospitali ya Tumbi.
Hata hivyo, aligoma kutibiwa kwenye hospitali hiyo akitaka ndugu zake wawepo.
Habari zinasema baadaye alisafirishwa kuhamishiwa Hospitali ya Amana kabla ya kuhamishwa tena na kwenda Muhimbili jana saa 9:00 alasiri.
Mfanyakazi mmoja wa Hospitali ya Amana aliiambia gazeti hili kuwa kabla ya askari wa Jeshi la Polisi kumfuata na gari mbili aina ya Land Rover, kundi la vijana wanaosadikiwa kuwa ni wahitimu wa mafunzo ya JKT, liliwasili Amana na kutaka kushinikiza kumchukua Mgoba, lakini uongozi uliwakatalia kwa maelezo kuwa wangetoa ruhusa hiyo kama wangekuwapo ndugu zake.
Alivyotekwa
Mwandishi wetu kutoka Kibaha anaripoti kuwa kijana huyo, anayejielezea kuwa ni mtetezi wa vijana waliohitimu JKT, aliokotwa kwenye kichaka kilichopo Picha ya Ndege mjini humo akiwa amejeruhiwa maeneo mbalimbali ya mwilini.

TAZAMA MATOKEO MAPYA YA KIDATO CHA NNE KATIKA SHULE ZA MBEYA




Friday, February 20, 2015

Ishu ya Mkuu wa Kituo cha Polisi kumbaka mahabusu Njombe

imagesMahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka  mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga kukiri kosa hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa kumtoa msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na kumbaka.
Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji.
Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rwezile amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.
Chanzo: Gazeti la Nipashe, Feb 20, 2015.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakat

LORI LA MAFUTA LAUA NA KUJERUHI TENA MBEYA


WATU WAWILI 1. MARIA PAJELA [18] NA 2. WILLIAM S/O PASCHAL [38] ,WOTE WAKAZI WA KIJIJI  CHA IDWELI, KATA YA ISONGOLE, TARAFA YA UKUKWE WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA, WALIFARIKI DUNIA BAADA YA KUUNGUA MOTO KIJIJINI HAPO JANA.


TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI LEO, IMESEMA KUWA, KATIKA TUKIO HILO MAREHEMU HAO PAMOJA NA BAADHI  YA WANANCHI WENGINE WA KIJIJI HICHO WALIKUWA KATIKA HARAKATI ZA KUIBA MAFUTA KUTOKA KATIKA GARI T.891 AQZ /T.821 ARF AINA YA SCANIA MALI YA AILIS SANGA LILILOKUWA LIMEBEBA MAFUTA AINA YA PETROLI UJAZO WA LITA 41,000, LIKITOKEA DSM KUELEKEA NCHINI MALAWI,  LIKIENDESHWA NA DEREVA ZAWADI NYATO [46] MKAZI WA SAE MBEYA AKIWA NA TINGO WAKE FRANK YOHANA [24],MKAZI WA MBOZI.

AWALI KABLA YA TUKIO HILO GARI HILO LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA, HIVYO WAHANGA [DEREVA NA TINGO] WALIFANIKIWA KUOKOLEWA NA KUPELEKWA KITUO CHA POLISI KIWIRA ILI KUPATA HATI YA MATIBABU [PF3] KWA AJILI YA KWENDA HOSPITALINI KUPATIWA MATIBABU. HATA HIVYO BAADHI YA WANANCHI WA ENEO HILO WALIVAMIA GARI HILO NA KUFANIKIWA KUTOBOA TANKI LA MAFUTA, HALI ILIYOPELEKEA MAFUTA KUANZA KUMWAGIKA/KUSAMBAA MAENEO HAYO NA HATA KUELEKEA MAENEO YENYE MAKAZI YA WATU  NA WAO KUKINGA KWA KUTUMIA VYOMBO VYAO.


KATIKA TUKIO HILO WATU KUMI NA NANE [18] WALIJERUHIWA, KATI YAO WANAUME NI 13 NA WANAWAKE 05 AMBAO NI: 1. SHUKURU KANZALE [21], 2. NURU GEORGE [30], 3.ASANTE BONIFACE [38], 4. JOSEPH JAMSON [18], 5.JOSEPH PASCHAL [30], 6.SIZA KANESA [22], 7.ALEX  DAUD [35], 8. OSCAR YOSIA [23], 9.TRAIPHON MOASI [37], 10.SAMSON MBWILA [29].

WENGINE NI 11. DORA MICHAEL [35],12. VERONICA ELIA [30],13.RABSEN AYUB [26], 14.WASIWASI SPIKA [32], 15.ASIA ANON [20], 16.BAHATI KYANDO [23], 17. CHRISTOPHER ERASTO [32] NA 18. MELISA SANANE [50], WOTE WAKAZI WA KIJIJI CHA IDWELI. AIDHA KATI YA MAJERUHI HAO,MAJERUHI 16 WAMELAZWA HOSPITALI YA MISHENI –IGOGWE NA MAJERUHI WAWILI WAMELAZWA HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA-TUKUYU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI.

Wednesday, February 18, 2015

Wapiganaji 300 wa Boko Haram wauawa

  jeshi la Nigeria limesema kuwa limewauwa zaidi ya wapiganaji 300 wa Boko Haram, baada ya jeshi la nchi hiyo kutwaa tena miji kadhaa iliyotekwa na wapiganaji hao kazkazini mashariki mwa Monguno.
Msemaji wa jeshi Chris Olukolade amesema kuwa wapiganaji wachache wa kiislamu pia wamekamatwa.
Bado hakujatolewa taarifa zaidi kuthibitisha habari hizo.
Mataifa kadhaa ya magharibi mwa Afrika kama vile Niger, Chad na Cameroon, ambayo yanakabiliana na Boko Haram pia yametoa taarifa ya maafa makubwa kwa kundi hilo ambalo limeleta kero kubwa katika ukanda huo.
Siku ya jumatatu wiki hii jeshi la Nigeria lilisema kuwa limeutwaa tena mji wa Monguno, ambao ulikuwa umetekwa na wapiganaji hao wa jihadi mwezi uliopita.

Tuesday, February 17, 2015

SIMANZI: AJINYONGA BAADA YA MATOKEO YAKE YA FORM 4 KUWA MABAYA.. MUANGALIE HAPA


Imekuwa kawaida kila mwaka pale ambapo matokeo yanapotoka watu wengi hutarajia mambo mazuri h ata yulealiye kuwa kilaza darasani naye anaamini atafaulu tu, ila matokeo yake mambo yanakuja kutokana na kile ulichopanda kama ulipanda mawe basi ni mawe unatakiwa kuvuna.
Kinachosikitisha Zaidi ni pale wanapo chukua hatua kama huyu
Kijana mmoja ajulikanae kwa jina John Maduhu wa Kijiji cha Pandagichiza, Wilaya ya Shinyanga vijijini kaamua kujinyonga baada ya matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka jana kumjia vibaya, akiongea na mwandishi, kaka wa marehemu alisema kuwa baada ya matokeo kutoka, John alitoweka nyumbani


                                        Mungu atusaidie na atusamehe kwa dhambi hizi