Tuesday, April 28, 2015




Monday, April 27, 2015

Ajira Mpya za Walimu Kwa Mwaka 2015 Zimetoka......Bofya Hapa Kuona Majina


A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya
 
Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa kama ifuatavyo:-
 
i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366;
 
ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari
 
iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari


B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
 
i. walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14 wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;
 
ii. kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya kazi;
 
iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;
 
iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na
 
v. fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa magari (ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya kuripoti.
 

Sunday, April 26, 2015

CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi


Mnamo tarehe 24/4/2015 huko maeneo ya Sogea Tunduma Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, METHEUS ANGANILE MWAFONGO, Mndali, 37yrs, Mkuu wa Ulinzi CDM Wilaya Momba, pamoja SALEHE TABLEI@SICHALWE, 22yrs, mkazi wa Majengo Tunduma walikamatwa kutokana na taarifa za kiintelijensia.

 
Watu  hawa walikamatwa wakiwa na buti pair 2 za kijeshi, kofia pair 2 za kijeshi, kamba kurukia ya mazoezi, vyuma kwa ajili ya mazoezi ya pushup, visu pair 2 kimoja spring knife na kingine kisu kikubwa, miwani ya FFU(ya kwenye misafara), manati pair 2 na mawe yake 40 pamoja na nati 4 zilizotarajiwa kutumiwa kama mawe, shenguard kwa ajili ya mikono na miguu pair 4, Bendera 2 za CDM, Tshirt 1 ya CDM, Kilemba 1, koti 1, Pamoja na barua 3 za CDM za kata ya MSANGANO, SHITETE, na KAMSAMBA (W) MOMBA zenye kichwa cha habari "UTOAJI WA VIONGOZI WA RED BRIGED KATIKA KATA YENU KWA MAFUNZO YA RED BRIGED". 
 
Barua inasomeka hivi
Husika na kichwacha barua hapo juu chajifafanua vema.


Napenda kukujulisha kuwa kutakuwa na ziara ya kimafunzo ya RB (Red Briged) katika kata yenu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi wa kumi mwaka huu.


Na kwa barua hii naomba uwapokee na uwape ushilikiano wa kutosha kwa ajili ya maendeleo ya chama chetu.


Ni matumaini yangu kuwa utawapokea na kuwatunza pamoja na usalama wao.


Wako katibu wa chama Wilaya.

 
Katika mahojiano vijana hawa walikuwa wakienda kutoa mafunzo ya kijeshi katika kata tajwa na mpango wao ni kufundisha vijana 300 katika wilaya ya Momba na mpango huu ni wa mkoa na Nchi nzima chini ya Mkurugenzi wa Usalama Taifa CDM bwana LWAKATARE.






WATU 20 WAKAMATWA NA POLISI KWA KUMSHUSHIA KIPIGO ASKARI POLISI HUKO MOROGORO

WATU 20 wamekamatwa na Polisi baada ya kumjeruhi askari aliyekuwa doria. 

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema watu hao 20 wanatuhumiwa kumpiga na kitu butu kichwani Askari Polisi mwenye namba F 3328 Cpl Ramadhani akiwa kwenye doria na mwenzake.

Pia kamanda huyo alisema Polisi inamshikilia mkazi wa Mawenzi mjini hapa, Dikanyo Ramadhani (29) kwa kupatikana na kete 87 za dawa za kulevya aina ya heroin ambazo thamani yake haikuweza kujulikana mara moja.

Mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 23, mwaka huu majira ya saa nne usiku katika maeneo ya Soko kuu la Manispaa ya Morogoro.

Alisema Polisi waliokuwa doria maeneo hayo walimtilia shaka mtu huyo na baada ya kumpekua kwenye mifuko yake ya suruali walimkuta akiwa na kete hizo 87.

Akizungumzia tukio la kupigwa askari, Kamanda huyo alisema watu 20 wakazi wa Mindu na Sangasanga, Manispaa ya Morogoro walimshambulia kwa kumpiga na kitu butu kichwani askari wa jeshi hilo mwenye namba F 3328 Koplo Ramadhani.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo, askari huyo baada ya kupigwa na watu hao alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro ambako amelazwa na anaendelea vizuri na matibabu.

Alisema kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 23, mwaka huu majira ya saa 4: 45 asubuhi eneo la Mindu, barabara kuu ya Morogoro- Iringa, Manispaa ya Morogoro, ambapo pikipiki isiyofahamika namba za usajili iliyokuwa ikiendeshwa na Juma Abasi (18), mkazi wa Mindu kuligonga gari lenye namba za usajili T 953 AQF aina ya Isuzu Tipper iliyokuwa ikiendeshwa na Joseph Laurent (28) , mkazi wa Modeco.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo pikipiki hiyo iliyokuwa ikitokea Mindu Bwawani kuelekea barabara ya Iringa, mwendeshaji wake alipowaona askari Polisi wawili waliokuwa doria maeneo hayo wakiwa na pikipiki, aligeuka ghafla na kuingia barabarani bila kuchukua hadhari na kuigonga gari hiyo iliyokuwa ikitokea Morogoro mjini kuelekea Sangasanga na kusababisha majeraha kwa mpanda pikipiki huyo.

Kamanda huyo wa Polisi wa mkoa alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mwendesha pikipiki huyo kuingia barabarani bila kuchukua tahadhari.

Hata hivyo alisema ajali hiyo ilishuhudiwa na askari hao waliokuwa doria na pikipiki maeneo hayo na hivyo walifika eneo la ajali ili kutoa msaada na katika harakati hizo za kutoa masaada ndipo askari Koplo Ramadhani alipopigwa na kitu butu kichwani na watu waliotokea eneo hilo na kuanguka chini.

Saturday, April 25, 2015

Muuguzi amchapa mjamzito viboko......Ni wakati wa uchungu wa kujifungua, Mtoto afia tumboni.


Muuguzi mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani Dodoma, amekumbwa na kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.

Aidha, mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa kuwa mbaya.

Mwanamke huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata mtoto wake akiwa hai.

Akisimulia mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy. 
 
“Nilishuhudia Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana,” alisema.

Alisema muuguzi huyo alitumia fimbo tatu kumchapa mgonjwa wake, ambazo alikuwa akizitumia kila moja inapovunjika. Alisema fimbo hizo zilipomalizika, alianza kumfinya kwenye mapaja kwa kutumia rula.

“Kesho yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu,” alisema.

Alisema Maroda alifikishiwa chumba cha upasuaji na kisha alilazwa wodi namba 17, lakini miguu na tumbo vilianza kuvimba na alipochunguzwa ikabainika ana usaha tumboni, hivyo aliamriwa arudishwe kwenye chumba cha upasuaji.
 
 “Yaani ukimuona, mwilini ana alama za fimbo na kufinywa. Sasa walipomfanyia upasuaji kwa awamu ya pili, alipelekwa ICU mpaka hivi tunavyozungumza ni zaidi ya wiki moja,” alieleza Charles.

Viongozi wa Hospitali ya Rufaa, wenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo walionekana ‘kurushiana mpira’ walipotakiwa kuelezea suala hilo. Hata hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo, alikiri kuwepo kwa mgonjwa huyo.

Awali Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula, alisema hakuwa na taarifa za kina kuhusu Maroda.
 
Mkindo alisema walikuwa wameagiza Ofisi ya Mganga wa Wilaya wa Chamwino, kuwapelekea taarifa kuhusu suala hilo.

Alisema pia wametaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, ifahamishwe hatua zilizochukuliwa dhidi ya mtumishi aliyedaiwa kumchapa viboko mjamzito huyo.

“Mimi sio msemaji, anayetakiwa kuwapa taarifa kamili ni RMO (Chaula) kwanini awalete kwangu, nilichowaeleza ni ambacho nafahamu lakini siyo msemaji, nashauri muende ofisini kwa matroni wa hospitali mtapata taarifa kamili,” alisema.

Afisa Muuguzi wa ICU, Christina Mlumba, alisema, Maroda alipelekwa ICU baada ya kufanyiwa upasuaji na kwamba hali yake inaendelea vizuri.

Mdogo wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa hakuingia kwenye chumba cha kujifungulia katika zahanati ya muungano, dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili tu, kwa sababu ya kudeka kwake.

Thursday, April 23, 2015

Mwili wa mwanafunzi Kiteto Aliyefariki Kwa Kuchapwa Viboko na Walimu wafikishwa Dodoma


MWILI wa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Matui iliyoko Wilaya ya Kiteto, Mkoa wa Manyara, aliyedaiwa kufariki baada ya kuchapwa viboko na walimu wake, Emmanuel Mbigima (15), umefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Wakati mwili huo unafikishwa hospitalini hapo jana asubuhi, ulikuwa umewekwa kwenye gari la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ukisindikizwa na baadhi ya ndugu wa karibu wa familia ya marehemu.

Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini hapo, babu wa marehemu, Emmanuel Ngowi, alisema mwili huo umeletwa hospitalini hapo kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ambavyo vimekosekana katika hospitali ya Wilaya ya Kiteto.

"Mjukuu wangu alipigwa na walimu watatu tarehe 20 mwezi huu kutokana na kufeli mtihani wa somo la Kiswahili.

“Tumechukua uamuzi wa kumleta hapa kwa sababu madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto, walishindwa kubaini kichwa kimeathirika kwa kiasi gani kwa kuwa hawana vifaa vya uchunguzi vya  kichwa.

“Hata hivyo, majibu ya uchunguzi wa awali yaliyotolewa katika hospitali hiyo, yalionyesha jicho la kulia lilivuja damu kwa ndani na pia mwili wa marehemu ulikuwa na michubuko miguuni,” alisema Ngowi.

Naye mjomba wa marehemu, Michael Ezekiel alisema matukio ya wanafunzi kupigwa na kupoteza maisha yamekuwa yakijirudia shuleni hapo kwa kuwa hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa.

“Mwaka jana kuna mtoto alipigwa na mwalimu akafariki, lakini mtuhumiwa alipelekwa mahakamani na baadaye kuachiwa kwa madai kuwa mtoto alikuwa ni mgonjwa,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk. Zainabu Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mwili huo na kusema uchunguzi bado unaendelea.

Awali, akizungumza na MPEKUZI baada ya mwanafunzi huyo kufariki, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime, aliwataja walimu waliohusika katika tukio hilo na ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, kuwa ni Machael Bajutta (28), Chalamilla Gereza (33) na Mwalimu Joyce Msiba (36).

Breaking News: Watu 10 Wafariki Dunia Baada ya Basi la kampuni ya Unique Kugongana na Gari la Coca Cola


Habari  zilizotufikia  zinaarifu  kuwa  basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.

Watu 10 wamefariki na  50 wamejeruhiwa.Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.


Picha  na  habari  ya  kina  itakuijia  baadaye.

Mengine kutoka Afrika Kusini pamoja na picha 12 hali ilivyokua

South Africa immigrant attacks
Mitandaoni kumekuwa na picha na video nyingi zimesambaa zikionesha hali ilivyokuwa Afrika Kusini kwa zaidi ya wiki moja, tumesikia na kuona mashambulizi ambayo wamefanyiwa watu ambao sio raia wa Afrika Kusini ndani ya nchi hiyo, video nyingi na picha zinasikitisha.. watoto wanauawa, wanajeruhiwa.. vurugu ilikuwa kubwa sana.
South Africa immigrant attacks
Hapa ni ndani ya Kambi ya muda ambayo wamehifadhiwa wageni, yani walikuwa na maisha yao kawaida tu mtaani baadae wanajikuta ni wakimbizi.
Cha mwisho kilichonifikia ni kuhusu ishu ya Waziri wa Usalama wa South Africa, Nosiviwe Mpisa-Nqkula kutangaza kwamba sasa wanaoingia kupambana na watu wanaofanya vurugu hizo ni wanajeshi baada ya kuonekana kama Polisi wameelemewa nguvu na hali ilivyo mitaani, watu saba waliripotiwa kufariki pia.
South Africa immigrant attacks
Baadhi ya watu waliokusanyika kulaani mashambulizi ya wageni ndani ya Afrika Kusini.
South Africa immigrant attacks
Mtaani hali haikuwa sawa, hili ni sehemu ya kundi kubwa la watu waliokuwa wanaandamana kupinga Xenophobia, ubaguzi wa kutaka wageni waondoke Afrika Kusini.
South Africa immigrant attacks
Akina mama na watoto wao, wako kwenye foleni kusubiri chakula cha msaada ndani ya Kambi ya wakimbizi ambayo wamehifadhiwa kwa muda.
South Africa immigrant attacks
Waandamanaji wakiwa na silaha, hali haikuwa shwari hata kidogo kwa wageni.
Askari wakiendelea na zoezi la kuwakamata watu wanaochochea mashambulizi ya wageni

South Africa immigrant attacks
South Africa immigrant attacks
Mmoja ya majeruhi akipatiwa huduma ya dharura ya matibabu.
South Africa immigrant attacks
Hali ilivyo kwenye Kambi walizohifadhiwa wageni

Foleni ya kupokea chakula cha msaada ndani ya Kambi

Waandamanaji na silaha zao mtaani
South Africa immigrant attacksSouth Africa immigrant attacksSouth Africa immigrant attacks

South Africa immigrant attacks
Mfalme wa Wazulu, Goodwill Zwelithini. Analaumiwa kusababisha machafuko yaliyotokea Afrika Kusini kutokana na kauli yake aliyoisema kwamba wageni wanatakiwa warudi kwao. Jumatatu April 22 amekanusha kushinikiza machafuko hayo
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe alisema kuna Watanzania waliouawa lakini mauaji hayo hayakutokana na vurugu hizi za kuwakataa wageni.
Pole kwa watu wetu wote ambao wameathirika kutokana na vurugu hizi.



No comments:

Post a Comment