Staa wa filamu za Bollywood kwenye Headlines kwa mara nyingine mahakamani!!
Mwaka 2002 mwigizaji filamu maarufu duniani wa Bollywood kutoka India Salman Khan,
alishtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari lake kwenye
kundi la watu waliokuwa wamelala kando ya barabara huku mmoja wa watu
hao akipoteza maisha.
Habari
mpya kwa sasa ni kwamba mahakama ya India imemuhukumu kifungo cha miaka
mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtu huyo huku akiwa
amelewa mjini Mumbai.
Khan amedai kuwa dereva wake ndiye
anapaswa kulaumiwa kwa tukio hilo lakini mashuhuda wanasema mwigizaji
huo ndiye aliyekuwa anaendesha gari na alikimbia baada ya kutokea kwa
ajali hiyo.
Baadhi ya filamu ambazo staa huyo aliweza kuigiza na kufanya vyema kwenye soko la filamu duniani ni pamoja na Dabangg, Ready, Bodyguard, Ek Tha Tiger na Maine Pyar Kiya.
No comments:
Post a Comment