MSANII FEROOZ ATIWA MBARONI KWA UTAPELI
Tena? Kwa mara nyingine staa wa Bongo Fleva, Ferooz Mrisho ametiwa mbaroni kwa utapeli akidaiwa ‘kuchikichia’ fedha za kumpangisha nyumba jamaa aliyejitambulisha kwa jina la Tony Noah kiasi cha zaidi ya Sh. milioni 3.2 kisha kuingia mitini ikielezwa kuwa nyumba hiyo ina mgogoro.
Kwa
mujibu wa chanzo chetu cha kuaminika, ilidaiwa kwamba, staa huyo
aliyewahi kutamba na Ngoma ya Starehe amekuwa na tabia ya kuwaingiza
watu mkenge kwa lengo la kutafuta mpangaji kwenye nyumba hiyo iliyopo
Sinza- Mori, Dar ambayo anaishi na ndugu zake.
Kilitiririka
kuwa, awali Ferooz alikuwa akitafuta mpangaji wa nyumba hiyo kupitia
kwa dalali ndipo Tony akavutiwa na nyumba hiyo na kukubaliana kutoa kodi
ya Sh. milioni 3, 250,000 kwa mwaka.Kilidai kwamba Tony alipomlipa
Ferooz fedha hiyo, Machi 14, mwaka huu ndipo akaanza kumpiga kalenda
ndipo aliamua kulipeleka shauri kwenye chombo cha sheria.
Kutokana
na sekeseke hilo, mwanahabari wetu alimtafuta Tony ambaye alisema kuwa,
baada ya kukubaliana na Ferooz kumpa fedha hizo na kuona anaanza
kumzungusha kuhamia kwenye nyumba hiyo alimwambia waandikishiane kwenye
Kituo cha Polisi Kijitonyama, Dar (Mabatini) kuwa atamlipa fedha hizo
Aprili 15 lakini Ferooz hakufanya hivyo.
Kutokana
na ishu hiyo, hadi gazeti hili linakwenda mtamboni, Ferooz alikuwa
ameshikiliwa Mabatini kwa jalada la kesi namba KJN/RB/3898/15 KUJIPATIA
FEDHA KWA NJIA YA UDANGANYIFU.Mwaka jana Ferooz alishikiliwa kituoni
hapo kwa msala wa kukamatwa na bangi.
Sunday, April 19, 2015
Mwalimu ajinyonga, mtendaji agongwa na kufariki papo hapo
Akizungumzia matukio hayo Kaimu Kamanda wa Polisi
mkoani hapa, Audax Mjaliwa alisema katika Mtaa wa Nyamatare Manispaa ya
Musoma, mwalimu Tengeru Mongu (43) wa Shule ya Msingi Igina wilayani
Serengeti alikutwa amejinyonga katika chumba cha binamu yake Mauma
Machunde.
Akisimulia mkasa huo binamu wa marehemu huyo
alisema, alipoamka jana asubuhi, alikwenda kumgongea mgeni wake huyo
bila mafanikio hali iliyomchanganya na kutoa taarifa kwa majirani
waliofika kumsaidia kuvunja mlango.
Machunde alisema, baada ya mlango kuvunjwa
alimkuta binamu yake akining’inia juu ya dari akiwa amejinyonga kwa
kutumia shuka na sababu za kujinyonga hazijajulikani kwani hakuacha
ujumbe wowote.
Mwalimu ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema, marehemu mwalimu huyo alipata uhamisho kutoka Serengeti kwenda Wilaya ya Butiama, uhamisho ambao aliuomba kwa madai kuwa umri alionao anafaa kufanyia kazi maeneo ya nyumbani kwao.
Mwalimu ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema, marehemu mwalimu huyo alipata uhamisho kutoka Serengeti kwenda Wilaya ya Butiama, uhamisho ambao aliuomba kwa madai kuwa umri alionao anafaa kufanyia kazi maeneo ya nyumbani kwao.
Katika tukio jingine basi lililosadikiwa kuwa ni
la Kampuni ya Peace Maker katika Barabara ya Bunda - Kiabakari kwenye
Kitongoji cha Kibisa, Kijiji cha Nyamisisi, Butiama limemgonga mtembea
kwa miguu jana usiku saa mbili usiku na kumsababishia kifo cha papo
hapo.
Akizungumzia ajali hiyo mtoto wa marehemu, Alfred
Kitambara, Veronika Kitambara alisema, baba yake ni Mtendaji wa Kata ya
Kyanyari na alipopata ajali hiyo alikuwa akitoka katika mkutano wa
kijiji akiwa anaendesha pikipiki.
Kitambara alisema, wakati baba yake akiwa njiani
alipata ajali ya pikipiki ambapo alipiga simu nyumbani na kumweleza mama
yake kuwa amepata ajali ya pikpiki amegonga jiwe akaanguka na kudai
kuwa hali yake siyo nzuri hivyo alimtaka mama kwenda kumsaidia.
“Wakati mama akiwa njiani alikutana na watu
wakisema kuwa basi limemgonga mtu lakini halijasimama sidhani kama mtu
huyo atakuwa amepona, kufika katika eneo la tukio alikuta aliyegongwa ni
baba lakini pikipiki ilikuwa mbali kwa maana hiyo alikuwa ameiacha
akawa anatembea ndiyo akagongwa,” alisema Kitambara mtoto wa marehemu.
Kaimu Kamanda wa Polisi alikiri kuwapo kwa tukio
hilo na kwamba polisi wanaendelea kuchunguza magari ya kampuni hiyo ili
kubaini ni gari lipi lililogonga kwa madai kuwa hakuna gari iliyofika
kituoni kutoa taarifa hizo.






No comments:
Post a Comment