Monday, April 27, 2015
Ajira Mpya za Walimu Kwa Mwaka 2015 Zimetoka......Bofya Hapa Kuona Majina
A: Orodha ya Walimu na Mafundi Sanifu Maabara Ajira Mpya
Ofisi
ya Waziri Mkuu - TAMISEMI inatangaza ajira ya wahitimu wa mafunzo ya
ualimu na mafundi sanifu maabara katika mamlaka ya Serikali za Mitaa
kama ifuatavyo:-
i. walimu wa cheti (Daraja IIIA) kwa ajili ya shule za msingi 11,366;
ii. walimu wa stashahada 4,151 na shahada 12,490 kwa ajili ya shule za sekondari
iii. mafundi sanifu maabara 264 kwa ajili kusimamia maabara na kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo katika shule za sekondari
B: Utaratibu Ajira Mpya kwa Walimu na Mafundi Sanifu Maabara
Kila mwajiriwa mpya anatakiwa kuzingatia yafuatayo:-
i.
walimu wenye sifa waliohitimu mafunzo kwa mwaka wa masomo 2013/14
wamepangwa pamoja na walimu wa sekondari wa masomo ya sayansi na
hisabati waliohitimu miaka ya nyuma na wameomba kuajiriwa;
ii.
kuripoti kuanzia tarehe 01 Mei hadi 09 Mei 2015 kwenye Ofisi za
Wakurugenzi wa Halmashauri kwa ajili ya kuajiriwa na kupangwa vituo vya
kazi;
iii. kuwasilisha vyeti halisi vya taaluma ya kuhitimu mafunzo, elimu ya sekondari, cheti cha kuzaliwa pamoja na nakala zake;
iv. hakutakuwa na mabadiliko ya vituo vya kazi; na
v.
fedha za kujikimu kwa muda wa siku saba (7) na nauli ya usafiri wa
magari (ground travel) zitatolewa kwenye halmashauri husika baada ya
kuripoti.
Sunday, April 26, 2015
CHADEMA Wakamatwa na Vifaa vya Kijeshi
Mnamo tarehe 24/4/2015 huko maeneo ya Sogea Tunduma Wilaya ya Momba Mkoa wa Mbeya, METHEUS ANGANILE MWAFONGO, Mndali, 37yrs, Mkuu wa Ulinzi CDM Wilaya Momba, pamoja SALEHE TABLEI@SICHALWE, 22yrs, mkazi wa Majengo Tunduma walikamatwa kutokana na taarifa za kiintelijensia.
Watu hawa walikamatwa wakiwa na buti pair 2 za kijeshi, kofia pair 2 za kijeshi, kamba kurukia ya mazoezi, vyuma kwa ajili ya mazoezi ya pushup, visu pair 2 kimoja spring knife na kingine kisu kikubwa, miwani ya FFU(ya kwenye misafara), manati pair 2 na mawe yake 40 pamoja na nati 4 zilizotarajiwa kutumiwa kama mawe, shenguard kwa ajili ya mikono na miguu pair 4, Bendera 2 za CDM, Tshirt 1 ya CDM, Kilemba 1, koti 1, Pamoja na barua 3 za CDM za kata ya MSANGANO, SHITETE, na KAMSAMBA (W) MOMBA zenye kichwa cha habari "UTOAJI WA VIONGOZI WA RED BRIGED KATIKA KATA YENU KWA MAFUNZO YA RED BRIGED".
Barua inasomeka hivi
Husika na kichwacha barua hapo juu chajifafanua vema.
Napenda kukujulisha kuwa kutakuwa na ziara ya kimafunzo ya RB (Red Briged) katika kata yenu kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi utakaofanyika mwezi wa kumi mwaka huu.
Na kwa barua hii naomba uwapokee na uwape ushilikiano wa kutosha kwa ajili ya maendeleo ya chama chetu.
Ni matumaini yangu kuwa utawapokea na kuwatunza pamoja na usalama wao.
Wako katibu wa chama Wilaya.
WATU 20 WAKAMATWA NA POLISI KWA KUMSHUSHIA KIPIGO ASKARI POLISI HUKO MOROGORO
WATU 20 wamekamatwa na Polisi baada ya kumjeruhi askari aliyekuwa doria.
Kamanda
wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Leonard Paulo alisema watu hao 20
wanatuhumiwa kumpiga na kitu butu kichwani Askari Polisi mwenye namba F
3328 Cpl Ramadhani akiwa kwenye doria na mwenzake.
Pia
kamanda huyo alisema Polisi inamshikilia mkazi wa Mawenzi mjini hapa,
Dikanyo Ramadhani (29) kwa kupatikana na kete 87 za dawa za kulevya aina
ya heroin ambazo thamani yake haikuweza kujulikana mara moja.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa Aprili 23, mwaka huu majira ya saa nne usiku katika maeneo ya Soko kuu la Manispaa ya Morogoro.
Alisema
Polisi waliokuwa doria maeneo hayo walimtilia shaka mtu huyo na baada
ya kumpekua kwenye mifuko yake ya suruali walimkuta akiwa na kete hizo
87.
Akizungumzia
tukio la kupigwa askari, Kamanda huyo alisema watu 20 wakazi wa Mindu
na Sangasanga, Manispaa ya Morogoro walimshambulia kwa kumpiga na kitu
butu kichwani askari wa jeshi hilo mwenye namba F 3328 Koplo Ramadhani.
Kwa
mujibu wa Kamanda huyo, askari huyo baada ya kupigwa na watu hao
alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro ambako
amelazwa na anaendelea vizuri na matibabu.
Alisema
kuwa tukio hilo lilitokea Aprili 23, mwaka huu majira ya saa 4: 45
asubuhi eneo la Mindu, barabara kuu ya Morogoro- Iringa, Manispaa ya
Morogoro, ambapo pikipiki isiyofahamika namba za usajili iliyokuwa
ikiendeshwa na Juma Abasi (18), mkazi wa Mindu kuligonga gari lenye
namba za usajili T 953 AQF aina ya Isuzu Tipper iliyokuwa ikiendeshwa na
Joseph Laurent (28) , mkazi wa Modeco.
Kwa
mujibu wa Kamanda huyo pikipiki hiyo iliyokuwa ikitokea Mindu Bwawani
kuelekea barabara ya Iringa, mwendeshaji wake alipowaona askari Polisi
wawili waliokuwa doria maeneo hayo wakiwa na pikipiki, aligeuka ghafla
na kuingia barabarani bila kuchukua hadhari na kuigonga gari hiyo
iliyokuwa ikitokea Morogoro mjini kuelekea Sangasanga na kusababisha
majeraha kwa mpanda pikipiki huyo.
Kamanda
huyo wa Polisi wa mkoa alisema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa
mwendesha pikipiki huyo kuingia barabarani bila kuchukua tahadhari.
Hata
hivyo alisema ajali hiyo ilishuhudiwa na askari hao waliokuwa doria na
pikipiki maeneo hayo na hivyo walifika eneo la ajali ili kutoa msaada na
katika harakati hizo za kutoa masaada ndipo askari Koplo Ramadhani
alipopigwa na kitu butu kichwani na watu waliotokea eneo hilo na
kuanguka chini.
Saturday, April 25, 2015
Muuguzi amchapa mjamzito viboko......Ni wakati wa uchungu wa kujifungua, Mtoto afia tumboni.
Muuguzi
mmoja wa zahanati ya Muungano, Chamwino, mkoani Dodoma, amekumbwa na
kashfa nzito baada ya kudaiwa kumchapa viboko mama mjamzito, wakati
akiwa katika hali ya uchungu wa kujifungua na kusababisha mtoto
aliyetaka kujifungua kufariki akiwa tumboni.
Aidha,
mama huyo ambaye kwa sasa amelazwa katika chumba cha uangalizi maalumu
(ICU) katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, hali yake inaelezwa
kuwa mbaya.
Mwanamke
huyo, Mariamu Maroda, anadaiwa kulazwa kwenye chumba hicho kwa zaidi ya
wiki moja, ambapo pamoja na kufanyiwa upasuaji, hakufanikiwa kupata
mtoto wake akiwa hai.
Akisimulia
mkasa huo, mama mdogo wa Maroda, Joyce Charles, alisema Aprili 3, mwaka
huu Saa 12:00 jioni, walimpeleka zahanati ya Muungano akiwa na dalili
za kujifungua na kupokelewa na muuguzi aliyemfahamu kwa jina la Lucy.
“Nilishuhudia
Lucy akimchapa Maroda viboko kwenye mapaja na mgongoni, akisema ana
uwezo wa kujifungua lakini anadeka tu, nilishindwa kuingilia nikihofia
asimdhuru zaidi mwanangu, ila nilihuzunika sana,” alisema.
Alisema
muuguzi huyo alitumia fimbo tatu kumchapa mgonjwa wake, ambazo alikuwa
akizitumia kila moja inapovunjika. Alisema fimbo hizo zilipomalizika,
alianza kumfinya kwenye mapaja kwa kutumia rula.
“Kesho
yake saa 12:00 alfajiri, huku hali ya mgonjwa ikiwa mbaya, walitupatia
gari likatupeleka hospitali ya Mvumi Misheni, ambako walisema hali
aliyokuwa nayo mgonjwa wasingeiweza na kutuelekeza tumpeleke hospitali
ya rufaa, lakini walimpa mgonjwa chupa mbili za damu,” alisema.
Alisema
Maroda alifikishiwa chumba cha upasuaji na kisha alilazwa wodi namba
17, lakini miguu na tumbo vilianza kuvimba na alipochunguzwa ikabainika
ana usaha tumboni, hivyo aliamriwa arudishwe kwenye chumba cha upasuaji.
“Yaani
ukimuona, mwilini ana alama za fimbo na kufinywa. Sasa walipomfanyia
upasuaji kwa awamu ya pili, alipelekwa ICU mpaka hivi tunavyozungumza ni
zaidi ya wiki moja,” alieleza Charles.
Viongozi
wa Hospitali ya Rufaa, wenye mamlaka ya kuzungumzia suala hilo
walionekana ‘kurushiana mpira’ walipotakiwa kuelezea suala hilo. Hata
hivyo, Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Anatoria Mkindo, alikiri kuwepo
kwa mgonjwa huyo.
Awali Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Zainab Chaula, alisema hakuwa na taarifa za kina kuhusu Maroda.
Mkindo alisema walikuwa wameagiza Ofisi ya Mganga wa Wilaya wa Chamwino, kuwapelekea taarifa kuhusu suala hilo.
Alisema
pia wametaka Ofisi ya Mganga Mkuu wa mkoa, ifahamishwe hatua
zilizochukuliwa dhidi ya mtumishi aliyedaiwa kumchapa viboko mjamzito
huyo.
“Mimi
sio msemaji, anayetakiwa kuwapa taarifa kamili ni RMO (Chaula) kwanini
awalete kwangu, nilichowaeleza ni ambacho nafahamu lakini siyo msemaji,
nashauri muende ofisini kwa matroni wa hospitali mtapata taarifa
kamili,” alisema.
Afisa
Muuguzi wa ICU, Christina Mlumba, alisema, Maroda alipelekwa ICU baada
ya kufanyiwa upasuaji na kwamba hali yake inaendelea vizuri.
Mdogo
wa Maroda, Silika Mkwawi alivieleza vyombo vya habari kuwa ingawa
hakuingia kwenye chumba cha kujifungulia katika zahanati ya muungano,
dada yake alipotolewa nje, muuguzi alimueleza kuwa alimchapa fimbo mbili
tu, kwa sababu ya kudeka kwake.
Thursday, April 23, 2015
Mwili wa mwanafunzi Kiteto Aliyefariki Kwa Kuchapwa Viboko na Walimu wafikishwa Dodoma
MWILI wa mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya Sekondari Matui iliyoko Wilaya ya Kiteto, Mkoa wa Manyara, aliyedaiwa kufariki baada ya kuchapwa viboko na walimu wake, Emmanuel Mbigima (15), umefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Wakati
mwili huo unafikishwa hospitalini hapo jana asubuhi, ulikuwa umewekwa
kwenye gari la Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto ukisindikizwa na baadhi
ya ndugu wa karibu wa familia ya marehemu.
Akizungumza
na waandishi wa habari hospitalini hapo, babu wa marehemu, Emmanuel
Ngowi, alisema mwili huo umeletwa hospitalini hapo kwa ajili ya
kufanyiwa vipimo ambavyo vimekosekana katika hospitali ya Wilaya ya
Kiteto.
"Mjukuu wangu alipigwa na walimu watatu tarehe 20 mwezi huu kutokana na kufeli mtihani wa somo la Kiswahili.
“Tumechukua
uamuzi wa kumleta hapa kwa sababu madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya
Kiteto, walishindwa kubaini kichwa kimeathirika kwa kiasi gani kwa kuwa
hawana vifaa vya uchunguzi vya kichwa.
“Hata
hivyo, majibu ya uchunguzi wa awali yaliyotolewa katika hospitali hiyo,
yalionyesha jicho la kulia lilivuja damu kwa ndani na pia mwili wa
marehemu ulikuwa na michubuko miguuni,” alisema Ngowi.
Naye
mjomba wa marehemu, Michael Ezekiel alisema matukio ya wanafunzi
kupigwa na kupoteza maisha yamekuwa yakijirudia shuleni hapo kwa kuwa
hakuna hatua zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa.
“Mwaka
jana kuna mtoto alipigwa na mwalimu akafariki, lakini mtuhumiwa
alipelekwa mahakamani na baadaye kuachiwa kwa madai kuwa mtoto alikuwa
ni mgonjwa,” alisema.
Kwa
upande wake, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk.
Zainabu Chaula, alithibitisha kupokelewa kwa mwili huo na kusema
uchunguzi bado unaendelea.
Awali,
akizungumza na MPEKUZI baada ya mwanafunzi huyo kufariki, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Manyara, Christopher Fuime, aliwataja walimu waliohusika
katika tukio hilo na ambao wanashikiliwa na Jeshi la Polisi, kuwa ni
Machael Bajutta (28), Chalamilla Gereza (33) na Mwalimu Joyce Msiba
(36).
Breaking News: Watu 10 Wafariki Dunia Baada ya Basi la kampuni ya Unique Kugongana na Gari la Coca Cola
Habari zilizotufikia zinaarifu kuwa basi la Unique lenye namba za usajili T148 BKK likitokea jijini Mwanza kwenda Tabora limegongana uso kwa uso na lori la kampuni la Cocacola katika kijiji cha Ibingo kata ya Samuye Shinyanga.
Watu 10 wamefariki na 50 wamejeruhiwa.Majeruhi wamekimbizwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Picha na habari ya kina itakuijia baadaye.
Mengine kutoka Afrika Kusini pamoja na picha 12 hali ilivyokua
Mitandaoni kumekuwa na picha na video
nyingi zimesambaa zikionesha hali ilivyokuwa Afrika Kusini kwa zaidi ya
wiki moja, tumesikia na kuona mashambulizi ambayo wamefanyiwa watu ambao
sio raia wa Afrika Kusini ndani ya nchi hiyo, video nyingi na picha
zinasikitisha.. watoto wanauawa, wanajeruhiwa.. vurugu ilikuwa kubwa
sana.

Hapa
ni ndani ya Kambi ya muda ambayo wamehifadhiwa wageni, yani walikuwa na
maisha yao kawaida tu mtaani baadae wanajikuta ni wakimbizi.
Cha mwisho kilichonifikia ni kuhusu ishu ya Waziri wa Usalama wa South Africa, Nosiviwe Mpisa-Nqkula kutangaza
kwamba sasa wanaoingia kupambana na watu wanaofanya vurugu hizo ni
wanajeshi baada ya kuonekana kama Polisi wameelemewa nguvu na hali
ilivyo mitaani, watu saba waliripotiwa kufariki pia.

Mtaani
hali haikuwa sawa, hili ni sehemu ya kundi kubwa la watu waliokuwa
wanaandamana kupinga Xenophobia, ubaguzi wa kutaka wageni waondoke
Afrika Kusini.

Akina
mama na watoto wao, wako kwenye foleni kusubiri chakula cha msaada
ndani ya Kambi ya wakimbizi ambayo wamehifadhiwa kwa muda.
Askari wakiendelea na zoezi la kuwakamata watu wanaochochea mashambulizi ya wageni
Foleni ya kupokea chakula cha msaada ndani ya Kambi
Waandamanaji na silaha zao mtaani



Mfalme wa Wazulu, Goodwill Zwelithini.
Analaumiwa kusababisha machafuko yaliyotokea Afrika Kusini kutokana na
kauli yake aliyoisema kwamba wageni wanatakiwa warudi kwao. Jumatatu
April 22 amekanusha kushinikiza machafuko hayo
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe alisema kuna Watanzania waliouawa lakini mauaji hayo hayakutokana na vurugu hizi za kuwakataa wageni.
Pole kwa watu wetu wote ambao wameathirika kutokana na vurugu hizi.