Mkali mwingine wa Bongo aliyeingia kwenye playlist ya video zinazoruka MTV Base !!
Kipindi
cha nyuma kidogo wakati muziki wa Tanzania ukianza kusikika nchi za
nje, tulikuwa tukiona kitu cha ajabu sana kwa vituo vikubwa vya nje
vikipiga muziki wetu.. wengi wetu tulikua na mawazo tofauti na kuona
kama jambo la ajabu hivi !
Tuliamini ili video za Bongo zifanye
vizuri kwenye television za nje basi ni lazima video hiyo itengenezwe na
directors kutoka nje pia, lakini kwa sasa tumeona video kadhaa za Bongo
zikipenya tena zikiwa zimeongozwa na directors wa hapa hapa TZ.
Ni furaha kumuona Barakah Da Prince ameiongeza namba ya video za Bongo zinazochezwa na vituo vikubwa duniani kwa sasa, video yake ambayo imeongozwa na Khalfan tayari imeanza kuchezwa na kituo cha MTV Base mtu wangu.
Video hiyo ya ‘Siachani Nawe‘ unaweza kuicheki hapa ukaenjoy kwa mara nyingine tena !!

No comments:
Post a Comment