Thursday, May 7, 2015

AJALI MBAYA TENA BASI LA NYAGAWA KUTOKA LITOKALO NJOMB-DAR LAPATA AJALI::soma zaid hapa




Basi la Nyagawa Express kutoka Njombe limepata ajali na kupinduka eneo la Mwidu Morogoro
Katika ajali hiyo watu watatu wanahofia wamepoteza maisha na majeruhi 15.

KONDA WA DALADALA MATATANI KWA KUISHI KINYUMBA NA HUYU MWANAFUNZI HAPA!


KONDAKTA wa daladala inayopiga kazi njia ya Makumbusho na Gongo la Mboto, jijini Dar aliyetambulika kwa jina moja la Saidi (pichani), ameingia matatani baada ya kudaiwa kuishi kinyumba na mwanafunzi wa kidato cha tatu, tukio lililotokea Magomeni Kagera hivi karibuni, kinyume na sheria za nchi.


Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizo, denti huyo mwenye umri wa miaka 17 anayesoma Shule ya Sekondari Nguvu Mpya, iliyopo Chanika,  Dar aliishi chumbani kwa konda huyo baada ya bibi yake anayeishi naye maeneo ya Sinza, Dar kusafiri kuelekea Zanzibar.
Ilidaiwa kuwa wawili hao wamekuwa wakiishi kama mke na mume tokea Machi,  mwaka huu ambapo konda huyo akitoka humfungia ndani.Ndani ya chumba cha konda huyo, waandishi wetu wakiwa na polisi, walishuhudia sare za shule pamoja na begi na madaftari na katika upekuzi kwenye madaftari hayo, ilionekana mara ya mwisho aliandika Machi, mwaka huu.

Hata hivyo, kondakta huyo hakuwepo nyumbani wakati wa tukio hilo, lakini polisi wameahidi kumsaka na kumkamata ili kumfikisha mbele ya sheria.Mwanafunzi huyo aliliambia Uwazi kuwa alikutana na konda huyo katika gari lake ambapo alikuwa akimpatia unafuu wa usafiri bila kunyanyaswa kama inavyowatokea wanafunzi wengine kabla ya kuanza uhusiano wa kimapenzi.


Alipoulizwa kuhusu wazazi wake, alidai mama yake alishafariki na hakuwahi kumuona baba yake, akidai anaishi na bibi yake maeneo ya Sinza, Dar ingawa hivi sasa amesafiri kwenda Zanzibar.

Inawezekana hiki alichokiandika Irene Uwoya @Instagram ni story yake ya ukweli na sio movie???

IRENE I
Inawezekana Irene Uwoya ameamua kuweka sehemu ya historia ya maisha yake kwenye ukurasa wake wa Instagram???
Sio kitu kigeni sana kuona mtu anafaya hivyo lakini post aliyoweka pamoja na picha yake huenda ina vitu vingine ambavyo hatukuwahi kujua kuhusu yeye.. ni staa wa movie, swali jingine ni hili; hii ni sehemu ya movie au ni true story ya kwake yeye kuhusu maisha yake??
Kama ni ishu ya kweli kabisa kuhusu maisha yake basi hii ni part 1, picha na kile allichoandika viko hapa.
irene
INAENDELEA...”bunge na kumaliza la saba!nikaenda kidato cha kwanza st.thomas gongolamboto mpaka kidato cha pili badae nikaenda Uganda nikasoma mpaka kidato cha 3 nikarud bongo kuchukua pass mpya coz yakwanza ilikuwa imesha isha…..ilikuwa ijumaaa nikiwa nimeenda kwajili ya pass mpya nirud shule!!!ndipo nilikutana na kaka mmoja mrefu,mweusi akaniita malaika”nikashangaa mhh mbona sio jina langu ?akanisogelea a kanambia kwa lugha ya kingereza Naitwa Patrick ponce monzanga!nikawa na nashangaaa coz sikuwa namjua’nikamwambia naitwa irene akanambia naomba nikwite malaika coz ur sooo beautiful huku akinipa mkono…nilipo mpa mkono tuuu basiii kumbe nilikuwa nimejitengenezea bomu bila kujua…..ITAENDELEAAAaaaaaaaaa“– @
IRENE I
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye fb

Mkali mwingine wa Bongo aliyeingia kwenye playlist ya video zinazoruka MTV Base !!

IMG-20150506-WA0010Kipindi cha nyuma kidogo wakati muziki wa Tanzania ukianza kusikika nchi za nje, tulikuwa tukiona kitu cha ajabu sana kwa vituo vikubwa vya nje vikipiga muziki wetu.. wengi wetu tulikua na mawazo tofauti na kuona kama jambo la ajabu hivi !
Tuliamini ili video za Bongo zifanye vizuri kwenye television za nje basi ni lazima video hiyo itengenezwe na directors kutoka nje pia, lakini kwa sasa tumeona video kadhaa za Bongo zikipenya tena zikiwa zimeongozwa na directors wa hapa hapa TZ.
IMG-20150506-WA0012Ni furaha kumuona Barakah Da Prince ameiongeza namba ya video za Bongo zinazochezwa na vituo vikubwa duniani kwa sasa, video yake ambayo imeongozwa na Khalfan tayari imeanza kuchezwa na kituo cha MTV Base mtu wangu.
IMG-20150506-WA0011
Video hiyo ya ‘Siachani Nawe‘ unaweza kuicheki hapa ukaenjoy kwa mara nyingine tena !!

Staa wa filamu za Bollywood kwenye Headlines kwa mara nyingine mahakamani!!

black
Mwaka 2002 mwigizaji filamu maarufu duniani wa Bollywood kutoka India Salman Khan, alishtakiwa kwa kuua bila kukusudia baada ya kuelekeza gari lake kwenye kundi la watu waliokuwa wamelala kando ya barabara huku mmoja wa watu hao akipoteza maisha.
Habari mpya kwa sasa ni kwamba mahakama ya India imemuhukumu kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mtu huyo huku akiwa amelewa mjini Mumbai.
khan
Salman Khan akiwa ndani ya gari huku akizingirwa na waandishi wa habari kabla ya kutolewa hukumu
Khan amedai kuwa dereva wake ndiye anapaswa kulaumiwa kwa tukio hilo lakini mashuhuda wanasema mwigizaji huo ndiye aliyekuwa anaendesha gari na alikimbia baada ya kutokea kwa ajali hiyo.
Baadhi ya filamu ambazo staa huyo aliweza kuigiza na kufanya vyema kwenye soko la filamu duniani ni pamoja na Dabangg, Ready, Bodyguard, Ek Tha Tiger na Maine Pyar Kiya.
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye TwitterFacebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata.