Magufuli Aahidi Ushindi wa Tsunami CCM......Asema Wapinzani Wataishia Kupiga Kelele Tu, Mwigulu Nchemba Naye Apigilia Msumari wa 'Moto'
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, amewahakikishia wana-CCM na Watanzaia kwa ujumla kuwa mwaka huu, chama kitapata ushindi wa Tsunami na si wa kishindo wala kimbunga.
Dk
Magufuli alisema hayo nje ya ofisi ya chama hicho mkoani Mtwara juzi
alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho ambapo alisisitiza
kuwa wapinzani watapiga kelele sana, wataongea sana lakini ushindi kwa
CCM ni lazima na upo pale pale.
Alisema
ushindi huo unatokana na matawi yaliyoanguka ndani ya chama na kuhama
na kwamba watu hao wameiacha CCM ikiwa safi na salama zaidi.
Alisema
watu hao walikuwa wakitumia fedha nyingi kurubuni watu wakati wa
mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ambapo chama kiliwakata na
kukimbilia vyama vingine vya upinzani.
Aliwataka
wana-CCM wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo na badala yake
washikamane, wawe kitu kimoja na kwamba mwaka huu, chama kitafanya
kampeni za kisayansi.
Aidha,
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema ni kazi rahisi
kumnadi Dk Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.
Mwigulu,
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alisema walioshindwa kwenye
mchakato wa kura za maoni na kuhama ndani ya chama, hivi sasa wanahaha
kutafuta urais wenyewe ambapo wanatoa mpaka hela ili kutafuta uongozi,
lakini wataumbuka mapema.
Akizungumza
na mamia ya wana-CCM waliojitokeza kumpokea katika hiyo ofisi ya chama
ambapo alifika kwa ajili ya kuwasalimia na kuwashukuru kwa kumchagua
kuwa mgombea na kumdhamini, Dk Magufuli aliwataka makada hao na
Wtanzania kwa ujumla kutoyumba kwa kuwa Watanzania walio wengi bado
wanakipenda Chama.
“Ushindi
wa mwaka huu wala si wa kimbunga ni wa Tsunami, watapiga kelele sana,
watakuja na propaganda nyingi sana, lakini ushindi wa CCM ni lazima. Ni
lazima tupate ushindi wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani,” alisema.
Alisema walikuwa watu 42, wakati wakiomba kuteuliwa na chama hivi sasa, CCM ina kundi moja tu la ushindi.
“Hako
ka tawi kamoja ndio kakameguka kwenda uko mbali, mti ambao unataka
upate mbao zake nzuri matawi kudondoka chini ni vizuri ili upate mbao
safi.
“Lakini baada ya kudondoka hilo ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama CCM.
"Hata
ukiangalia tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wapo
waliotoka wako akina Kambona walitoka na wengine walifukuzwa na wengine
walijua watafukuzwa wakakimbia wenyewe kabla ya kufukuzwa kama hao,” alisema.
Alisema
iwapo atachaguliwa kuongoza dola atapenda awe mtumishi wa watu,
asiyekuwa na majivuno ili aweze kuwatumikia wananchi na atimize
matarajio yao.
Dk
Magufuli alisema wakati wa kampeni ukifika zitafanyika za kistaarabu na
kisayansi na kwamba zitakuwa za shina kwa shina, tawi kwa tawi, kata
kwa kata, jimbo kwa jimbo, wilaya, mkoa na taifa.
Aliwataka wana-CCM wasimame imara kwani wananchi wengi wanakipenda Chama.
Dk
Magufuli akizungumzia uzoefu wake ndani ya CCM, alisema alikuwa mbunge
katika kipindi chake cha miaka 20, ambapo vipindi viwli alipita bila
kupingwa na alikuwa waziri kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali.
Alisema
anaifahamu vizuri Mtwara, Tanzania, CCM na kero za Watanzania
anazifahamu vya kutosha hivyo akipewa nafasi watashudia wenyewe kasi ya
utendaji kwa maendeleo ya taifa.
“Nilichaguliwa
na mkutano mkuu kutoka kila kona ya nchi kwa asilimia 87, wale
walionichagua waliwakishia Watanzania wote. Niwahakikishie kuwa mwaka
huu, tutashinda zaidi,” alisema.
Aliwataka
wana-CCM katika umoja wao kutulia na kutoyumbishwa na maneno ya porojo
kwa kuwa chama kinajiuliza kwa kile walichofanya kwa wananchi na si
maneno matamu bila vitendo.
“Chama
nakifahamu, shida za wana-CCM nazifahamu, matarajio yao nayafahamu,
shida za wananchi nazifahamu hivyo kama nitachaguliwa nitawatumikia kwa
uadilifu mkubwa ili kuwaletea maendeleo,” alisema.
Sunday, August 9, 2015
BENKI YA POSTA TANZANIA, YASAIDIA SHULE ZA MSINGI WILAYANI ILEJE MKOANI MBEYA
Naibu waziri wa
Viwanda na Biashara, Janet Mmbene, (wapili kushoto), akipeana mikono na Meneja
msaidizi wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, tawi la Tunduma, Teddy Msanzi, wakati
wa hafla ya kukabidhi madawati yaliyotolewa kama msaada na benki hiyo, kusaidia
shule mbili za msingi wilayani Ileje, mkoa wa Mbeya, hivi karibuni
Benki
ya Posta Tanzania (TPB) kupitia tawi lake la Tunduma, imetoa msaada wa madawati
100 yenye thamani ya shilingi Milioni Tatu kwa shule mbili za Msingi zilizopo
Wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
Akikabidhi
madawati hayo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene kwenye
hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Wilayani humo hivi karibuni, Meneja wa
Benki ya Posta Tawi la Tunduma Teddy Msanzi alisema kuwa, Benki yake iliguswa sana na suala la uhaba wa
madawati kwa wanafunzi wa Wilaya hiyo na kuona ni muhimu kusaidia.
“Benki
ya Posta inatambua umuhimu wa elimu bora kwa ajili ya kujenga kizazi bora cha
baadae. Ni vigumu kutoa elimu bora katika mazingira magumu ya wanafunzi kukaa
chini madarasani.Ni vema wanafunzi wetu wakawekewa mazingira mazuri ya kupata
elimu, ikiwemo madawati. Hivyo basi sisi Benki ya Posta tunatoa madawati haya
100 ili kupunguza tatizo hili.” Alifafanua Teddy.
Kwa
mujibu wa taarifa ya ofisi ya elimu wilaya Ileje, Wilaya hiyo ina jumla ya
wanafunzi 28,488 wa shule za Msingi , lakini idadi ya madawatii ni 10,028, na
kufanya idadi ya madawati yanayohitajika kuwa 4,116.
Akitoa
shukrani zake kwa niaba ya shule za Wilaya ya Ileje, Mhe. Janeth Mbene aliishukuru
Benki ya Posta kwa msaada huo ambao alisema ni mkombozi kwa wanafunzi waliokuwa
wakikaa chini kwa muda mrefu. Alitumia fursa hiyo pia kuziomba taasisi nyingine
ziguswe na tatizo lao na ziweze kuwasaidia ili waweze kuondokana na changamoto
hiyo.
Naibu Waziri Mmbene, akiwa na maafisa wa benki hiyo, tawi la Tunduma
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimkabidhi katibu wa CCM Wilaya ya
Ileje Hamida Mbogo madawati ya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi
wilayani ileje ambayo yametolewa na benki Posta Tawi la Tunduma.
Saturday, August 8, 2015
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA KUHITIMISHA SIKU YA NANE NANE JIJINI MBEYA
Hawa ni watu ambao wameweza kufika katika viwanja vya John Mwakangale kwa ajili ya kujionea mambo mbalimbali Nanenane
Baadhi
ya wanafunzi walionekana wakiwa kaika viwanja hivyo kwa ajili ya
kujifunza mbalimbali yahusuyo Kilimo, ufugaji na Mengine mengiiiii....
Wafanya Biashara nao hawakuwa mbali, kuumia fursa kupitia msimu wa nane nane.
Uuzaji wa Mitumba ni miongoni mwa shughuli zinazofanywa katika viwanja vya nane nane
Wengine hao wanaondoka
Thursday, July 30, 2015
PICHA: Lowassa Achukua Fomu ya Urais CHADEMA
Umati wa watu waliojitokeza kumpokea Lowassa wakati akichukua fomu ya urais kupitia Chadema.
…Akisaini katika kitabu cha wageni.
Mnadhimu Mkuu kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu akitoa yake machache.
Baada ya kuchukua fomu.
Mwenyekiti wa Chadema (kushoto)
Mhe. Freeman Mbowe Mhe. Edward Lowassa (katikati) wakati wa zoezi la
kuchukua fomu lililofanyika leo Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini
Dar .
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwa katika meza kuu ya Chadema.
**
**
WAZIRI MKUU wa zamani, Mhe. Edward Lowassa hivi punde amechukua fomu
ya kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Lowassa amekabidhiwa fomu hiyo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa,
Freeman Mbowe kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Lowassa alijiunga rasmi na Chadema juzi akitokea CCM baada ya
kuondolewa kwenye mchakato wa kuwa mgombea urais wa chama hicho akidai
kuwa jina lake liliondolewa kwa mizengwe.
No comments:
Post a Comment