kachuchu baby
one love
Thursday, August 18, 2016
Friday, August 14, 2015
Magufuli Aahidi Ushindi wa Tsunami CCM......Asema Wapinzani Wataishia Kupiga Kelele Tu, Mwigulu Nchemba Naye Apigilia Msumari wa 'Moto'
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, amewahakikishia wana-CCM na Watanzaia kwa ujumla kuwa mwaka huu, chama kitapata ushindi wa Tsunami na si wa kishindo wala kimbunga.
Dk
Magufuli alisema hayo nje ya ofisi ya chama hicho mkoani Mtwara juzi
alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho ambapo alisisitiza
kuwa wapinzani watapiga kelele sana, wataongea sana lakini ushindi kwa
CCM ni lazima na upo pale pale.
Alisema
ushindi huo unatokana na matawi yaliyoanguka ndani ya chama na kuhama
na kwamba watu hao wameiacha CCM ikiwa safi na salama zaidi.
Alisema
watu hao walikuwa wakitumia fedha nyingi kurubuni watu wakati wa
mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ambapo chama kiliwakata na
kukimbilia vyama vingine vya upinzani.
Aliwataka
wana-CCM wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo na badala yake
washikamane, wawe kitu kimoja na kwamba mwaka huu, chama kitafanya
kampeni za kisayansi.
Aidha,
Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema ni kazi rahisi
kumnadi Dk Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.
Mwigulu,
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alisema walioshindwa kwenye
mchakato wa kura za maoni na kuhama ndani ya chama, hivi sasa wanahaha
kutafuta urais wenyewe ambapo wanatoa mpaka hela ili kutafuta uongozi,
lakini wataumbuka mapema.
Akizungumza
na mamia ya wana-CCM waliojitokeza kumpokea katika hiyo ofisi ya chama
ambapo alifika kwa ajili ya kuwasalimia na kuwashukuru kwa kumchagua
kuwa mgombea na kumdhamini, Dk Magufuli aliwataka makada hao na
Wtanzania kwa ujumla kutoyumba kwa kuwa Watanzania walio wengi bado
wanakipenda Chama.
“Ushindi
wa mwaka huu wala si wa kimbunga ni wa Tsunami, watapiga kelele sana,
watakuja na propaganda nyingi sana, lakini ushindi wa CCM ni lazima. Ni
lazima tupate ushindi wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani,” alisema.
Alisema walikuwa watu 42, wakati wakiomba kuteuliwa na chama hivi sasa, CCM ina kundi moja tu la ushindi.
“Hako
ka tawi kamoja ndio kakameguka kwenda uko mbali, mti ambao unataka
upate mbao zake nzuri matawi kudondoka chini ni vizuri ili upate mbao
safi.
“Lakini baada ya kudondoka hilo ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama CCM.
"Hata
ukiangalia tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wapo
waliotoka wako akina Kambona walitoka na wengine walifukuzwa na wengine
walijua watafukuzwa wakakimbia wenyewe kabla ya kufukuzwa kama hao,” alisema.
Alisema
iwapo atachaguliwa kuongoza dola atapenda awe mtumishi wa watu,
asiyekuwa na majivuno ili aweze kuwatumikia wananchi na atimize
matarajio yao.
Dk
Magufuli alisema wakati wa kampeni ukifika zitafanyika za kistaarabu na
kisayansi na kwamba zitakuwa za shina kwa shina, tawi kwa tawi, kata
kwa kata, jimbo kwa jimbo, wilaya, mkoa na taifa.
Aliwataka wana-CCM wasimame imara kwani wananchi wengi wanakipenda Chama.
Dk
Magufuli akizungumzia uzoefu wake ndani ya CCM, alisema alikuwa mbunge
katika kipindi chake cha miaka 20, ambapo vipindi viwli alipita bila
kupingwa na alikuwa waziri kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali.
Alisema
anaifahamu vizuri Mtwara, Tanzania, CCM na kero za Watanzania
anazifahamu vya kutosha hivyo akipewa nafasi watashudia wenyewe kasi ya
utendaji kwa maendeleo ya taifa.
“Nilichaguliwa
na mkutano mkuu kutoka kila kona ya nchi kwa asilimia 87, wale
walionichagua waliwakishia Watanzania wote. Niwahakikishie kuwa mwaka
huu, tutashinda zaidi,” alisema.
Aliwataka
wana-CCM katika umoja wao kutulia na kutoyumbishwa na maneno ya porojo
kwa kuwa chama kinajiuliza kwa kile walichofanya kwa wananchi na si
maneno matamu bila vitendo.
“Chama
nakifahamu, shida za wana-CCM nazifahamu, matarajio yao nayafahamu,
shida za wananchi nazifahamu hivyo kama nitachaguliwa nitawatumikia kwa
uadilifu mkubwa ili kuwaletea maendeleo,” alisema.
Sunday, August 9, 2015
BENKI YA POSTA TANZANIA, YASAIDIA SHULE ZA MSINGI WILAYANI ILEJE MKOANI MBEYA
Naibu waziri wa
Viwanda na Biashara, Janet Mmbene, (wapili kushoto), akipeana mikono na Meneja
msaidizi wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, tawi la Tunduma, Teddy Msanzi, wakati
wa hafla ya kukabidhi madawati yaliyotolewa kama msaada na benki hiyo, kusaidia
shule mbili za msingi wilayani Ileje, mkoa wa Mbeya, hivi karibuni
Benki
ya Posta Tanzania (TPB) kupitia tawi lake la Tunduma, imetoa msaada wa madawati
100 yenye thamani ya shilingi Milioni Tatu kwa shule mbili za Msingi zilizopo
Wilayani Ileje, mkoani Mbeya.
Akikabidhi
madawati hayo kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Janeth Mbene kwenye
hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika Wilayani humo hivi karibuni, Meneja wa
Benki ya Posta Tawi la Tunduma Teddy Msanzi alisema kuwa, Benki yake iliguswa sana na suala la uhaba wa
madawati kwa wanafunzi wa Wilaya hiyo na kuona ni muhimu kusaidia.
“Benki
ya Posta inatambua umuhimu wa elimu bora kwa ajili ya kujenga kizazi bora cha
baadae. Ni vigumu kutoa elimu bora katika mazingira magumu ya wanafunzi kukaa
chini madarasani.Ni vema wanafunzi wetu wakawekewa mazingira mazuri ya kupata
elimu, ikiwemo madawati. Hivyo basi sisi Benki ya Posta tunatoa madawati haya
100 ili kupunguza tatizo hili.” Alifafanua Teddy.
Kwa
mujibu wa taarifa ya ofisi ya elimu wilaya Ileje, Wilaya hiyo ina jumla ya
wanafunzi 28,488 wa shule za Msingi , lakini idadi ya madawatii ni 10,028, na
kufanya idadi ya madawati yanayohitajika kuwa 4,116.
Akitoa
shukrani zake kwa niaba ya shule za Wilaya ya Ileje, Mhe. Janeth Mbene aliishukuru
Benki ya Posta kwa msaada huo ambao alisema ni mkombozi kwa wanafunzi waliokuwa
wakikaa chini kwa muda mrefu. Alitumia fursa hiyo pia kuziomba taasisi nyingine
ziguswe na tatizo lao na ziweze kuwasaidia ili waweze kuondokana na changamoto
hiyo.
Naibu Waziri Mmbene, akiwa na maafisa wa benki hiyo, tawi la Tunduma
Naibu
Waziri wa Viwanda na Biashara Janet Mbene akimkabidhi katibu wa CCM Wilaya ya
Ileje Hamida Mbogo madawati ya kwa ajili ya shule za sekondari na msingi
wilayani ileje ambayo yametolewa na benki Posta Tawi la Tunduma.
- life always is change from black to white I give congratulation 4 those who support me up this time.
Saturday, August 8, 2015
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA KUHITIMISHA SIKU YA NANE NANE JIJINI MBEYA
Hawa ni watu ambao wameweza kufika katika viwanja vya John Mwakangale kwa ajili ya kujionea mambo mbalimbali Nanenane
Baadhi
ya wanafunzi walionekana wakiwa kaika viwanja hivyo kwa ajili ya
kujifunza mbalimbali yahusuyo Kilimo, ufugaji na Mengine mengiiiii....
Wafanya Biashara nao hawakuwa mbali, kuumia fursa kupitia msimu wa nane nane.
Uuzaji wa Mitumba ni miongoni mwa shughuli zinazofanywa katika viwanja vya nane nane
Wengine hao wanaondoka
Thursday, July 30, 2015
PICHA: Lowassa Achukua Fomu ya Urais CHADEMA
Umati wa watu waliojitokeza kumpokea Lowassa wakati akichukua fomu ya urais kupitia Chadema.
…Akisaini katika kitabu cha wageni.
Mnadhimu Mkuu kambi rasmi ya upinzani bungeni, Tundu Lissu akitoa yake machache.
Baada ya kuchukua fomu.
Mwenyekiti wa Chadema (kushoto)
Mhe. Freeman Mbowe Mhe. Edward Lowassa (katikati) wakati wa zoezi la
kuchukua fomu lililofanyika leo Makao Makuu ya Chadema Kinondoni jijini
Dar .
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa akiwa katika meza kuu ya Chadema.
**
**
WAZIRI MKUU wa zamani, Mhe. Edward Lowassa hivi punde amechukua fomu
ya kuwania nafasi ya urais kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema).
Lowassa amekabidhiwa fomu hiyo na Mwenyekiti wa Chadema Taifa,
Freeman Mbowe kwenye ofisi za Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo
Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Lowassa alijiunga rasmi na Chadema juzi akitokea CCM baada ya
kuondolewa kwenye mchakato wa kuwa mgombea urais wa chama hicho akidai
kuwa jina lake liliondolewa kwa mizengwe.
Dk Slaa aikana twitter inayomzushia mazito
Wakati kukiwa na taarifa zinazosambaa mtandaoni zikimuhusisha Dk Willibrod Slaa na akaunti ambayo imekuwa ikitoa msimamo wake wa kujitenga na shughuli za siasa pamoja na Ukawa, katibu huyo mkuu wa Chadema amekanusha taarifa hizo akisema hajawahi kuwa na akaunti ya twitter.
Dk
Slaa, aliyekuwa anatajwa kuwa mgombea urais wa Chadema, hajaonekana
hadharani katika matukio makubwa ya kichama tangu Chadema na Ukawa
walipomkaribisha waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa na kumteua kuwa
mgombea urais anayeungwa mkono na vyama vinne vinavyounda umoja huo.
Mara
ya mwisho kuonekana kwenye shughuli za chama hicho ni katika kikao cha
Kamati Kuu wakati Lowassa alikaribishwa kufanya majadiliano na kujibu
hoja za wajumbe.
Lakini
baada ya hapo Dk Slaa hakuonekana wakati wa kutambulishwa kwa Lowassa
kwa waandishi wa habari, tukio la kuchukua na kurudisha fomu za urais
ndani ya chama na tukio la juzi la kuchukua fomu za urais kutoka Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Wakati
hayo yakiendelea, kuna akaunti ya twitter yenye jina la “Dr Willibrord
Slaa” ambayo imekuwa ikitoa kauli mfululizo zikiwa na ujumbe mbalimbali
unaoendana na mazingira aliyomo sasa mwanasiasa huyo.
Agosti 10, kulitumwa ujumbe zaidi mara 10, mmojawapo ukijaribu kuwaaminisha watu kuwa hiyo ni akaunti halisi ya Dk Slaa.
“Ndugu
zangu Watanzania, hii ni akaunti yangu rasmi, bila shaka yoyote na
naomba ninachoandika hapa kifikishwe kwa Watanzania popote walipo,” unasema ujumbe huo.
Taarifa
nyingine zilizotumwa kwenye akaunti hiyo ya twitter ni pamoja na ile
iliyoeleza kuwa Dk Slaa ameomba ulinzi kutoka nchi na mashirika ya
kimataifa na atazungumza kupitia runinga na redio pindi atakapopata
ulinzi.
Akizungumzia sakata hili jana, Dk Slaa alisema hajawahi kutuma taarifa yoyote kwenye mitandao ya kijamii.
“Sijawahi ku-operate (kuendesha) kitu chochote kwenye akaunti ya twitter, sina akaunti kama hiyo,” alisema Dk Slaa.
Mbali
na kukanusha kumiliki na kuendesha akaunti hiyo, Dk Slaa alirudia kauli
yake ya wiki iliyopita kuwa atatoa msimamo wake muda muafaka
utakapofika, baada ya kuulizwa swali kuhusu hatma yake ndani ya Chadema
na kisiasa kwa ujumla.
“Subira yavuta heri, sasa ili uipate hiyo heri unatakiwa kuvumilia. Kwa hiyo wakati ukifika nitazungumza tu na Watanzania,” alisema.
Alipoulizwa
ni wapi alipo kwa sasa, alisema yupo Dar es Salaam anapumzika, lakini
akasisitiza kuwa ipo siku ataweka wazi mustakabali wake kisiasa.
Dk
Slaa alisema yeye na mke wake Josephine Mushumbusi wanatarajia kusafiri
kwenda nje ya nchi katika siku chache zijazo, ingawa hakuweka wazi nchi
anayotarajia kuitembelea, lakini akasema atarejea baada ya wiki moja.
TUKIO LA KUSIKITISHA : RUNGWE AUAWA KINYAMA NA KUTUPWA KADO YA BARABARA

Tukio hilo limetokea wilayani rungwe mkoani Mbeya kata ya Katumba. Marehemu anasadikika kuwa ni mkazi wa Wilayani Ileje Mkoani Mbeya.
Pia inasemekana kuwa marehemu ametupwa sehemu hiyo usiku wa kuamkia leo na watu wasiosemekana kwa kutumia Usafiri wa bodaboda.
Picha zaidi.
Thursday, July 23, 2015
Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo
Taarifa
kutoka mkoani Dodoma zinasema watu zaidi ya 10 wamefariki dunia
usiku wa kuamkia leo , huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada
ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka
Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na
kisha kupinduka.
MFAHAM MGOMBEA WA UBUNGE KURA ZA MAONI MBEYA MJINI MCHAPAKAZ MPIGANAJI NDUGU SHADRACK MAKOMBE

Jumatano, 27 Mei 2015
MAAFISA SITA WA NGAZ YA JUU YA SHIRIKISHO LA KABUMBU ULIMWENGUN FIFA WAMEKAMATWA
Maafisa
sita wa ngazi ya juu wa shirikisho la kabumbu ulimwenguni
FIFA,wamekamatwa na maafisa wa vyombo vya sheria vya Uswisi hii leo
mjini Zurich,siku mbili kabla ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo.Maafisa
hao wanakabiliwa na kitisho cha kuhamishiwa Marekani.Huko watakabiliwa
na madai ya kuhusika na visa vya udanganyifu,ukandamizaji,na kubadilisha
fedha kinyume cha sheria.Kwa mujibu wa idara ya sheria ya serikali kuu
ya Uswisi,maafisa hao wa FIFA wanakabiliwa na tuhuma za kupokea
rushwa ya mamilioni ya dola tangu mwaka 1990 kutoka vyombo vya habari
za spoti na makampuni ya zana za spoti.Badala yake makampuni hayo
yamepatiwa ruhusa ya kuripoti,kusimamia na kushughulikia masuala ya
kibiashara katika michuano ya kabumbu nchini Marekani na Amerika ya
kusini.Mwenyekiti wa FIFA,Joseph Blatter si miongoni mwa watuhumiwa.
Bwana huyo mwenye umri wa miaka 79 atapigania kuchaguliwa upya ijumaaa
ijayo kuliongoza shirikisho hilo la dimba ulimwenguni.
BENK YA MAENDELEO YA AFRICA INAANDAA MKUTANO.....
Benki
ya maendeleo ya Africa, inaandaa mkutano wake wa kila mwaka huku
ikiadhimisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake. Hapo kesho benki hiyo
itamchagua rais wake mpya atakayechukua nafasi iliokuwa ikishikiliwa na
Donald Kaberuka raia wa Rwanda. Je ni mafanikio ya aina gani
yaliopatikana barani Africa tangu kuanzishwa kwa benki hiyo?
MNYAMA WA AJABU WAGUNDULIWA TANZANIA.....
Tanzania iliyobalikiwa
Mnyama wa ajabu agunduliwa Tanzania - "Tembomilia"Kwa mara ya kwanza askari wa wanyamapori katika mbuga ya Serengeti nchini Tanzania wamemgundua mnyama huyu waliyempa jina la "Tembomilia" na wanasayansi wanasema ni mara ya kwanza kwa kiumbe cha aina hii kuonekana duniani. Hivi sasa walinzi hao wa wanyamapori na wanasayansi wanamuhifadhi mnyama huyu wa ajabu, ambaye wanasayansi tayari wamempa jina la kitaalamu la "Tembomilia Tanzanianicus". Jina lenyewe la "Tembomilia" linatokana na maneno ya Kiswahili "tembo" na "pundamilia". Tembomilia aliyegunduliwa sasa ni wa dume akiwa na umri unaokisiwa kuwa miaka miwili na uzito wa kilo 520.
Na sasa ikiwa umeamini habari hii, basi tumefanikiwa kukushika kwenye mzaha wa Aprili Mosi.
Imechapishwa na
DIAMOND NA UTAJIRI WAKE WOTE ILA KAMWE HATAMFIKIA DAVIDO KWA UTAJIRI. HIZI NDO MALI ZA KIFAHARI ZA DAIVIDO. BOFYA HAPA
The Nigerian singer, who is undoubtedly one
of the richest in his country, is living the high life. From private
jets to fast cars and poshy residences, this dude is living the life.
The BET winner, MTV-EMA and MOBO Nominee is known for his lavish
spending stunts and occasional tweefs with his counterpart, Wiz Kid.
David Adedeji Adeleke as he is called by birth name, lives a trendy
lifestyle and is one of the most sought for musicians in Africa.Check out some the clothes, cars and homes he owns below:
Jumamosi, 9 Mei 2015
FWATILIA MOMBO MUIMU KWA KUJUAA KIONGOZ BORA NA BORA KIONGOZ KWA KIJANA ALIYE TANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE MBEYA MJINI SHEQ SHADRACK MAKOMBE
Nipe fursa
Katika mjadala huu,kumekuwepo na upotoshaji mkubwa wenye ni ovu ya kuchafua haiba za watu.
Dr.Slaa akiwa mwana ccm kwa umri wake wote wa ujana na kiongozi wa Tanu
Youth League aliposhindwa uchaguzi wa kura ya maoni mwaka 1995 aliamua
kuhamia Chadema na kumwacha Mkewe akiitumikia chadema lkn hakuwahi
huitwa Msaliti.
Tundu Lissu alikuwa Mwana ccm kindakindaki na baadae kutimkia NCCR
ambako nako hakudumu na kuhamia Chadema lkn hakuna aliemwita Msaliti.
Benson Kigaila alikuwa Kiongozi wa UDP na baadae kihamia chadema ambako
sasa ni mkurugenzi wa Oparation na Mafunzo na anaitwa kamanda licha ya
kuhama chama.
Lema alikuwa chama cha NCCR baadae akahama na Mrema kwenda TLP na baada
ya kuona imekufa akatimkia chadema ,leo anaitwa kamanda na si Msaliti.
Mabere Marando alikuwa mwana ccm baadae akawa katibu mkuu wa NCCR
mageuzi na hatimae akahamia Chadema ambako amewahi kuwa mwanasheria mkuu
wa chama kabla hajatiliwa mashaka na kuondolewa haraka.leo ni kamanda
na si Msaliti.
Prof.Abdallah Jumbe safari alikuwa kiongozi wa chama cha wananchi CUF na
baadae akajiunga na chadema lkn hakuitwa msaliti licha ya kuwa
alijiunga wakati CUF ikiwa chama kikuu cha upinzani nchini.
Orodha ni ndefu sana ....hao ni kwa uchache tu.
Sasa hoja yangu ni kuwa hivi karibuni kumeanzishwa Chama Kipya cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo)
Chama hiki kama vilivyo vyama vingine vilivyoanzishwa baada ya
ccm,kinategemea kupata wanachama toka vyama mbalimbali na wale wasiokuwa
na vyama.
Wapo walitoka ccm,ADC,CUF,NCCR-Mageuzi,n.k
Lkn hawa wakihamia ACT-husikii malalamiko(huenda wanatokea vyama vilivyokomaa kidemokrasia)
Kelele na maneno ya Usaliti hutolewa pake mwanachama anapohama toka chadema kwenda ACT.
Je kwanini CUF walitulia na kumtakia mausha mazuri ya kisiasa Prof Safari badala ya kuituhumu chadema?
Kwanini Ninyi hamjifunzi kwa waliotangulia kwenye siasa?
Hata wale waliohama ACT na kurudi chadema Mbona sisikii ACT wakilalamika?
Siasa ni kama Mpira,Mchezaji unaemtegemea anahamia kwa hasimu wako na bado haiwi mwisho wa Timu.
Rejea kadhia ta Van Persie kuhamia Man U,Tambwe Kuhamia Yanga,na Okwi kichezea Simba na baadae Yanga na sasa Simba tena.
Tuufunge Mjadala kwa kila chama kurudi kwenye malengo ya uanzishwaji wake.
Chadema fufueni M4C muendelee na mapambano kivyenu.
ACT-Wazalendo nao waendelee na Oparation zao za kuhakikisha nchi inarudi kwenye misingi ya kuasisiwa kwake.
CUF nao waendelee na kuhakikisha Tanzania inatoa haki sawa kwa wote n.k
Tunatofautiana Ideology japo focus ni kuondoa unyonyaji wa ccm.
Tunatofautiana Ideology japo focus ni kuondoa unyonyaji wa ccm.
Majangili,Wauza unga,Mafisadi na kila waovu wa nchi hii wananufaika na mgawanyiko wa Upinzani.
Foward ever,Backward
Hahahahah
daima huwa napenda sera za USA kwani kwao kiongozi bora ni yule aliye
jikomboa kifikra na kiuchumi ndio kiongozi bora na si vinginevyo WATANZANIA wanahitaji viongozi wanaokuja na solution na co viongozi wanaokuja na matatizo kama sehemu ya jamii

Subscribe to:
Posts (Atom)