Thursday, July 23, 2015

Ajali Mbaya ya Basi la Simiyu Express Yaua Watu Wengi Dodoma Usiku wa Kuamkia Leo


Taarifa kutoka mkoani Dodoma zinasema watu  zaidi  ya 10  wamefariki dunia usiku wa kuamkia leo , huku zaidi ya abiria 40 wakijeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya SIMIYU EXPRESS walilokua wakisafiria kutoka Mwanza kwenda DSM kupasuka tairi na kuacha njia na kugonga mbuyu na kisha kupinduka.
 
Taarifa zinasema ajali hiyo ni mbaya sana kuwahi kutokea mkoani Dodoma.Majeruhi wamekimbizwa katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu.

MFAHAM MGOMBEA WA UBUNGE KURA ZA MAONI MBEYA MJINI MCHAPAKAZ MPIGANAJI NDUGU SHADRACK MAKOMBE

Jumatano, 27 Mei 2015

MAAFISA SITA WA NGAZ YA JUU YA SHIRIKISHO LA KABUMBU ULIMWENGUN FIFA WAMEKAMATWA

Maafisa sita wa ngazi ya juu wa shirikisho la kabumbu ulimwenguni FIFA,wamekamatwa na maafisa wa vyombo vya sheria vya Uswisi hii leo mjini Zurich,siku mbili kabla ya mkutano mkuu wa shirikisho hilo.Maafisa hao wanakabiliwa na kitisho cha kuhamishiwa Marekani.Huko watakabiliwa na madai ya kuhusika na visa vya udanganyifu,ukandamizaji,na kubadilisha fedha kinyume cha sheria.Kwa mujibu wa idara ya sheria ya serikali kuu ya Uswisi,maafisa hao wa FIFA wanakabiliwa na tuhuma za kupokea rushwa ya mamilioni ya dola tangu mwaka 1990 kutoka vyombo vya habari za spoti na makampuni ya zana za spoti.Badala yake makampuni hayo yamepatiwa ruhusa ya kuripoti,kusimamia na kushughulikia masuala ya kibiashara katika michuano ya kabumbu nchini Marekani na Amerika ya kusini.Mwenyekiti wa FIFA,Joseph Blatter si miongoni mwa watuhumiwa. Bwana huyo mwenye umri wa miaka 79 atapigania kuchaguliwa upya ijumaaa ijayo kuliongoza shirikisho hilo la dimba ulimwenguni.

BENK YA MAENDELEO YA AFRICA INAANDAA MKUTANO.....

Benki ya maendeleo ya Africa, inaandaa mkutano wake wa kila mwaka huku ikiadhimisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake. Hapo kesho benki hiyo itamchagua rais wake mpya atakayechukua nafasi iliokuwa ikishikiliwa na Donald Kaberuka raia wa Rwanda. Je ni mafanikio ya aina gani yaliopatikana barani Africa tangu kuanzishwa kwa benki hiyo?

MNYAMA WA AJABU WAGUNDULIWA TANZANIA.....

Tanzania iliyobalikiwa
Mnyama wa ajabu agunduliwa Tanzania - "Tembomilia"
Kwa mara ya kwanza askari wa wanyamapori katika mbuga ya Serengeti nchini Tanzania wamemgundua mnyama huyu waliyempa jina la "Tembomilia" na wanasayansi wanasema ni mara ya kwanza kwa kiumbe cha aina hii kuonekana duniani. Hivi sasa walinzi hao wa wanyamapori na wanasayansi wanamuhifadhi mnyama huyu wa ajabu, ambaye wanasayansi tayari wamempa jina la kitaalamu la "Tembomilia Tanzanianicus". Jina lenyewe la "Tembomilia" linatokana na maneno ya Kiswahili "tembo" na "pundamilia". Tembomilia aliyegunduliwa sasa ni wa dume akiwa na umri unaokisiwa kuwa miaka miwili na uzito wa kilo 520.
Na sasa ikiwa umeamini habari hii, basi tumefanikiwa kukushika kwenye mzaha wa Aprili Mosi.

DIAMOND NA UTAJIRI WAKE WOTE ILA KAMWE HATAMFIKIA DAVIDO KWA UTAJIRI. HIZI NDO MALI ZA KIFAHARI ZA DAIVIDO. BOFYA HAPA

The Nigerian singer, who is undoubtedly one of the richest in his country, is living the high life. From private jets to fast cars and poshy residences, this dude is living the life. The BET winner, MTV-EMA and MOBO Nominee is known for his lavish spending stunts and occasional tweefs with his counterpart, Wiz Kid.
David Adedeji Adeleke as he is called by birth name, lives a trendy lifestyle and is one of the most sought for musicians in Africa.

Check out some the clothes, cars and homes he owns below:






WEMA SEPETU ATAZIMIA AKIZIONA PICHA HIZI ZA IDRIS AKIWA NA SAMANTHA WAKE>>>>.TEAM WEMA TU WAKOMENT

..



Jumamosi, 9 Mei 2015

FWATILIA MOMBO MUIMU KWA KUJUAA KIONGOZ BORA NA BORA KIONGOZ KWA KIJANA ALIYE TANGAZA NIA KUGOMBEA UBUNGE MBEYA MJINI SHEQ SHADRACK MAKOMBE

Nipe fursa
Katika mjadala huu,kumekuwepo na upotoshaji mkubwa wenye ni ovu ya kuchafua haiba za watu.
Dr.Slaa akiwa mwana ccm kwa umri wake wote wa ujana na kiongozi wa Tanu Youth League aliposhindwa uchaguzi wa kura ya maoni mwaka 1995 aliamua kuhamia Chadema na kumwacha Mkewe akiitumikia chadema lkn hakuwahi huitwa Msaliti.
Tundu Lissu alikuwa Mwana ccm kindakindaki na baadae kutimkia NCCR ambako nako hakudumu na kuhamia Chadema lkn hakuna aliemwita Msaliti.
Benson Kigaila alikuwa Kiongozi wa UDP na baadae kihamia chadema ambako sasa ni mkurugenzi wa Oparation na Mafunzo na anaitwa kamanda licha ya kuhama chama.
Lema alikuwa chama cha NCCR baadae akahama na Mrema kwenda TLP na baada ya kuona imekufa akatimkia chadema ,leo anaitwa kamanda na si Msaliti.
Mabere Marando alikuwa mwana ccm baadae akawa katibu mkuu wa NCCR mageuzi na hatimae akahamia Chadema ambako amewahi kuwa mwanasheria mkuu wa chama kabla hajatiliwa mashaka na kuondolewa haraka.leo ni kamanda na si Msaliti.
Prof.Abdallah Jumbe safari alikuwa kiongozi wa chama cha wananchi CUF na baadae akajiunga na chadema lkn hakuitwa msaliti licha ya kuwa alijiunga wakati CUF ikiwa chama kikuu cha upinzani nchini.
Orodha ni ndefu sana ....hao ni kwa uchache tu.
Sasa hoja yangu ni kuwa hivi karibuni kumeanzishwa Chama Kipya cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo)
Chama hiki kama vilivyo vyama vingine vilivyoanzishwa baada ya ccm,kinategemea kupata wanachama toka vyama mbalimbali na wale wasiokuwa na vyama.
Wapo walitoka ccm,ADC,CUF,NCCR-Mageuzi,n.k
Lkn hawa wakihamia ACT-husikii malalamiko(huenda wanatokea vyama vilivyokomaa kidemokrasia)
Kelele na maneno ya Usaliti hutolewa pake mwanachama anapohama toka chadema kwenda ACT.
Je kwanini CUF walitulia na kumtakia mausha mazuri ya kisiasa Prof Safari badala ya kuituhumu chadema?
Kwanini Ninyi hamjifunzi kwa waliotangulia kwenye siasa?
Hata wale waliohama ACT na kurudi chadema Mbona sisikii ACT wakilalamika?
Siasa ni kama Mpira,Mchezaji unaemtegemea anahamia kwa hasimu wako na bado haiwi mwisho wa Timu.
Rejea kadhia ta Van Persie kuhamia Man U,Tambwe Kuhamia Yanga,na Okwi kichezea Simba na baadae Yanga na sasa Simba tena.
Tuufunge Mjadala kwa kila chama kurudi kwenye malengo ya uanzishwaji wake.
Chadema fufueni M4C muendelee na mapambano kivyenu.
ACT-Wazalendo nao waendelee na Oparation zao za kuhakikisha nchi inarudi kwenye misingi ya kuasisiwa kwake.
CUF nao waendelee na kuhakikisha Tanzania inatoa haki sawa kwa wote n.k
Tunatofautiana Ideology japo focus ni kuondoa unyonyaji wa ccm.
Majangili,Wauza unga,Mafisadi na kila waovu wa nchi hii wananufaika na mgawanyiko wa Upinzani.
Foward ever,Backward Hahahahah daima huwa napenda sera za USA kwani kwao kiongozi bora ni yule aliye jikomboa kifikra na kiuchumi ndio kiongozi bora na si vinginevyo    WATANZANIA wanahitaji viongozi wanaokuja na solution na co viongozi wanaokuja na matatizo kama sehemu ya jamii